HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 9, 2017

JUMUIYA WATU WA CHINA YAULETA MPIRA WA ASIDE 5 NCHINI

Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii 
JUMUIYA ya Watu wa China nchini Tanzania kwa kushirikiana na Watanzania wameandaa tamasha la michezo ikiwa sehemu kudumisha umoja na ushirikiano wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

Tamasha hilo linahusisha michezo mbalimbali na kivutio kikubwa kilikuwa kwenye mchezo wa mpira wa Aside 5 ambao kwa hapa nchini bado haujafahamika zaidi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa tamasha hilo lililofanyika Uwanja wa Ndani eneo la Uwanja wa Taifa ,Katibu wa Siasa wa Ubalozi wa China nchini,Yang Tong amesema kuwa nchi hizo mbili zinatambua umoja na mshikamano uliopo kwa muda mrefu na anafurahia kuona ukiimarika siku hadi siku.

Amesema kwa kutumia tamasha hilo ambalo linahusisha jumuiya ya Watu wa China na Watanzania ni fursa nyingine ya kuendelea kudumisha urafiki uliopo kwenye nchi hizo kwa muda mrefu.

Tong amesema  michezo huleta watu pamoja na hivyo nchi hizo mbili wameendelea kutumia michezo kama sehemu mojawapo ya kutumisha urafiki uliopo.

Mashindano ya mpira huo yanayoendelea kwenye uwanja huo yamekuwa yakifanyika kila mwaka katika mwezi wa 12 na imekuwa chachu kubwa ya kudumisha tamaduni za nchi hizo mbili.

Nae Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Michezo wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Alex Nkenyenge amesema tamasha hilo ni muhimu na Jumuiya ya Watu wa China nchini Tanzania imetumia Sh milioni 35 kwa ajili ya ukarabati wa uwanja wa ndani wakati wakifanya maandalizi ya tamasha hilo.

Ametumia nafasi hiyo kusisitiza kuwa mbali ya kushiriki kwenye michezo China imekuwa ikijikita kwenye masuala ya uwekezaji na moja ya faida zake ni kutoa ajira kwa Watanzania.

"Jumuiya ya Watu wa China imekuwa ikishirikiana na Serikali yetu kwenye mambo mbalimbali yakiwamo ya uchumi na udamaduni.Hili ni jambo ambalo linapaswa kuendelezwa,"amesema.

Wakati huohuo Mchezaji wa zamani wa timu ya Tanzania 'Taifa Stars' ambaye pia amewahi kuwa Kocha wa timu hiyo Boniface Mkwasa amefafanua mpira wa Aside 5 hautofautiani sana na mpira wa miguu zaidi ya kwamba mchezo huo kiwanja chake ni kidogo na unachezwa kwa dakika chache.

Amesema ni wakati muafaka kwa Watanzania na hasa wapenda michezo wakajifundisha aina hiyo ya mpira kwan itatoa nafasi ya wao kupata soko la ajira kwani ni mchezo ambao unaonanekana kukua kwa kasi licha ya kwamba kwa Tanzania bado haujafahamika zaidi.

Pia Makamu Mwenyekiti wa Sun Shine Group Betty Mkwasa amesema tamasha hilo la mpira wa Aside 5 linafaida nyingi kwani ni sehemu ya kuimarisha urafiki wa nchi hizo mbili lakini pia inatoa nafasi ya ajira kwa Watanzania.

Amesema Kampuni ya Sun Shine Group mbali ya kushiriki mashindano hayo yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Watu wa China, pia wamekuwa wakishiriki kwenye mabonanza yanayohusisha kampuni yao ambayo ipo kwenye mikoa mbalimbali nchini.
 Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Michezo wa Wizara habari , Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex Nkeyenge akizungumza katika uzinduzi Tamasha la michezo kati ya Tanzania na China lilofanyika katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
 Mchezaji wa zamani na Kocha wa Timu ya Taifa Stars, Boniface Mkwasa akizungumza juu ya mchezo wa mpira wa miguu wa A side 5 uliochezwa katika katika tamasha la michezo kati ya Tanzania  na China  leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa Siasa wa Ubalozi wa China nchini,Yang Tong akizungumza katika tamasha la michezo kati ya Jumuiya ya watu wa china na Tanzania juu  uhusiano wa Tanzania na China ambao kwa sasa unakwenda hadi katika michezo, leo jijini Dar es Salaam. 
 Jumuiya ya watu wa china pamoja na watanzania wakiwa na mabango mbalimbali ya kampuni za China zilizopo nchini ambazo zimeshiriki tamasha la michezo kati ya Jumuiya ya Watu wa China na Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa karate wakionyesha umahiri wao katika tamasha la michezo kati ya Jumuiya ya Watu wa China na Tanzania leo jijini Dar es Salaam.
Kikundi cha mziki cha jumuiya ya watu wa china wakionyesha umahiri wao katika tamasha la michezo kati ya jumuiya ya watu wa china na Tanzania leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad