HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, December 25, 2017

BABA ASHIKILIWA KWA MAUAJI YA MWANAE

Jeshi la Polisi Mkoani Tabora  linawashikila watu watatu akiwemo baba mzazi wa mtoto Leokadia Maganga, mwenyekiti pamoja na mtendaji wa kata ya Ndala wilaya ya Nzega mkoani Tabora, kwa tukio la mauaji ya mtoto huyo mwenye umri wa miaka 11.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora Kamishna Msaidizi Muandamizi wa Polisi (SACP), Wilbroad Mutafungwa amesema mtoto huyo inadaiwa aliuwawa na kutumbukizwa kwenye kisima cha maji katika kijiji cha Budushi kata ya Ndala wilayani Nzega Mkoani Tabora.

"Ni kweli tulipokea taarifa za tukio hilo la mtoto kukutwa katika kisima cha maji na baadae kuzikwa, tuliamua kwenda mahakamani kuomba hati ya kufukua maiti ili tufanye uchunguzi, baba mzazi wa mtoto huyo bado tunamshikila  kwa ajili ya upelelezi", amesema Kamanda Mutafungwa.

Sambamba na hilo Kamanda Mutafugwa amewaomba wananchi wawe wavumilivu katika kipindi hiki  ambacho Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi, ili kubaini chanzo zaidi cha mtoto huyo kufariki, na mara utakapokamilika watatoa taarifa zaidi ya tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad