HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 30 November 2017

WAKULIMA NA WAFUGAJI BADO CHANGAMOTO, NAIBU WWZIRI ULEGA AAGIZA WAFUGAJI KUFUATA SHERIA


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Abdalaah Ulega akimsikiliza moja ya wafugaji wa Kijiji cha Matanzi Kata ya Beta wakati wa ziara yake katika Jimbo la Mkuranga akisikiliza changamoto za wananchi wake.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Ili kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (mb) Abdalah Ulega amewataka wafugaji wote waliongia vijijini kinyume cha sheria kufuata sheria vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa zidi yao.

Hayo ameyasema Mkuranga mkoani pwani wakati alipofanya ziara ya kutembelea vijiji vya jimboni kwake kuangalia changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo ambapo moja ya changamoto hizo ni tatizo la wakulima na wavugaji.

Aidha ulega amesema moja ya sababu ya migogoro ya wakulima na wafugaji ni kutokuwa na matumizi bora ya ardhi hivyo ameitaka jamii kuwa na matumizi bora ya ardhi ilikuweza kuepuka migogoro inayoweza kutokea.

"tatizo hakuna matumizi bora ya ardhi na ni lazima kuwe na matumizi bora ya ardhi pamoja na kupima maeneo ili maeneo ya wafugaji yaweze kujulikana",alisema

Amesema yeye kama Waziri atazungumza na watalaamu kutoka wizarani ili waweze kushirikiana na wataalamu wa halmashauri ya mkuranga kwa pamoja waweze kwenda katika kijiji cha Matanzi kutafuta ufumbuzi wa kudumu juu ya tatizo la wakulima na wafugaji.
Hata hivyo amemuagiza Afisa Mifugo wa kata ya Beta kuhakikisha ng'ombe wote wanapigwa chapa ili kuweza kujua idadi kamili ya ng'ombe na ametoa wito kwa wakulima na wafugaji kuhakikisha wanashirikiana,wanapenda,wavumiliane na waishi kwa amani. 

Awali wanachi wa kijiji cha Matanzi wakitoa malalamiko yao mbele ya Naibu Waziri huyo wamesema kijiji chao kilipokea kaya nne za wafugaji ambazo zina tambulika wakiwa na mifugo isiyozidi 300 lakini mpaka sasa kaya hizo zimeongezeka kinyume na utaratibu na idadi ya ng'ombe kuwa zaidi ya 900 hali inayopelekea mifugo kuwa mingi na kusambaa kwenye mashamba ya wakulima na kuharibu mazao yao.

Mbali na changamoto hiyo, katika ziara ya Naibu Waziri amekutana na ukosefu wa walimu katika kata ya Mkwechembe na Matanzi na kumuagiza Afisa Elimu wa Wilaya kuhakikisha walimu wanaongezwa kwenye shule hizo, pia ameshukuru Bruda Marcos kwa hatua kubwa aliyoifanya ya kujenga madarasa manne ya Shule ya Msingi Mkwechembe.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Abdallah Ulega akikagua shule ya Mkwechembe iliyojengwa na mfadhili Bruda Marcos katika Kijiji cha Mkwechembe.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Abdallah Ulaga akipokea zawadi kutoka kwa wanakijiji cha Mkwechembe wakati wa ziara yake kwenye Jimbo lake la Mkuranga jana Mkoani Pwani.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi (Mb) Abdallah Ulega akisalimiana na wanakijii wakati wa ziara ya Jimbo la Mkuranga jana Mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad