HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 15, 2017

TADB YAOMBWA ‘KUSAPOTI’ WADAU WA UFUGAJI WA SAMAKI

Na mwandishi wetu, Mwanza
Wadau wa tasnia ya ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba (fish caging) mkoani Mwanza wameiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuwasaidia katika kuendeleza tasnia iyo kwa kuwapatia mikopo na mahitaji mengine kwa ajili ya kuongeza tija katika ufugaji wa kisasa wa samaki mkoani humo.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa  Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju, Bw. Elpidius Mpanju Akizungumza wakati ugeni kutoka TADB ulipotembelea kujionea maendeleo ya tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba mkoani Mwanza.
Bw. Mpanju alisema kuwa ukosefu na ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha za mtaji kwa ajili ya maendeleo ya kilimo hasa katika tasnia hiyo mpya ya ufugaji wa samaki imekuwa inawapa changamoto katika uendelezaji wa tasnia hiyo yenye faida lukuki kwa maendeleo ya kiuchumi nchini.
Bw. . Mpanju aliongeza kuwa ukosefu wa mikopo ya uhakika imekuwa inarudisha nyuma ukuaji wa tasnia hiyo mpya nchini kwa kuwa mahitaji mengi kwa ajili ya kuhudumia ufugaji wa samaki inapatikana nje ya nchi hivyo kuhitaji kiasi kikubwa cha mtaji.
sekta ya mifugo na kurudisha nyuma juhudi za serikali katika kuendeleza sekta ya mifugo.
“Uduni na ukosefu wa mitaji ya uhakika inachangiwa kwa kiasi kikubwa na mikopo mingi kutoka taasisi za fedha kuelekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kutusahau sisi wakulima na wafugaji, hivyo tunaiomba TADB kutusaidia kutatua changamoto hii,” alisema.
Akijibu changamoto hizo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila alisema kuwa Serikali iliamua kuanzisha Benki ya Kilimo ili kusaidia kukabiliana na mapungufu ya wakulima nchini kote ili kuhuisha upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo na kuchagiza mapinduzi katika  kilimo nchini.
Bibi Kurwijila aliongeza kuwa tasnia ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba ni mojawapo ya minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani mazao na mifugo mbalimbali hasa katika uongezaji wa thamani wa ufugaji wa samaki nchini.
Aliongeza kuwa Benki ya Kilimo imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Samaki na uvuvi nchini ili ziweze kuchangia ukuaji wa uchumi nchini.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Chacha amesema kuwa TADB inatoa mikopo ya aina tatu ambayo ni Mikopo ya Muda Mfupi (Hadi Miaka Miwili (2), Mikopo ya Muda wa Kati (Zaidi ya Miaka 2 hadi Miaka Mitano (5)) na Mikopo ya Muda Mrefu (Zaidi ya Miaka 5 hadi Miaka Kumi na Mitano (15)).
“Mikopo hii ni ya riba nafuu ambayo inalenga katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka   kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (mbele) akiongoza Ujumbe kutoka Benki hiyo walipotembelea Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju lililopo Luchelele, mkoani Mwanza.
 Mkurugenzi wa  Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju, Bw. Elpidius Mpanju (kulia) akiuelezea Ugeni kutoka TADB kuhusu tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba.. wanaomsikiliza ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (wapili kulia), Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa Benki hiyo, Bw. Augustino Matutu Chacha (katikati). Wengine pichani ni wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bw. Joseph Mutashubilwa (kushoto) na Bw. Dome Malosha (wapili kushoto).
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bibi Rosebud Kurwijila (kulia) akihoji masuala mbalimbali kuhusu tasnia ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba wakati alipouongoza ugeni kutoka TADB kutembelea Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju lililopo Luchelele, mkoani Mwanza. Wanaomsikiliza ni Mmiliki wa kampuni hiyo, Bw. Anuruphus Mpanju (kushoto), Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (wapili kushoto) na Mkurugenzi wa  Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju, Bw. Elpidius Mpanju (kulia).
 Meneja Mradi wa Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju, Bw. Artem Ivanieiev (kushoto) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Biashara na Mikopo wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha (kulia) kuhusu Shamba la Kutotoleshea vifaranga vya samaki vya Kampuni ya Mpanju.
 Ugeni kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania wakiangalia namna ya vifaranga vya samaki vinavyohudumiwa kwenye Shamba la Ufugaji wa Samaki la Mpanju lililopo Luchelele, mkoani Mwanza.
Sehemu ya vizimba vya kukuzia samaki vinavyomilikiwa na Kampuni ya Ufugaji wa Samaki ya Mpanju.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad