HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 28 November 2017

Taasisi ya JKCI kwa kushirikiana na Taasisi ya OHI ya nchini Australia wafanya upasuaji wa Moyo kwa watoto na watu wazima

 Afisa Muuguzi kutoka Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia  Lisa Heywood akibadilishana mawazo na Emma Thomas  na Faustina Mwapinga ambao wote ni Maafisa Uuguzi  wakati wa kambi ya upasuaji wa moyo ya siku tano inayoendelea katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Katika kambi hiyo wagonjwa 23 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua  kati ya hao watoto 13 na watu wazima 10. 
  Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia  wakimfanyia upasuaji wa moyo mtoto wa miezi sita ambaye mishipa yake ya  moyo ilikuwa na tatizo la kupeleka damu kwa wingi kwenye mapafu wakati wa kambi maalum ya siku tano inayoendelea JKCI. Hadi sasa jumla ya watoto watano na watu wazima wawili wameshafanyiwa upasuaji.
Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na mishipa ya damu  kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) wakati wa kambi maalum ya upasuaji ya siku tano inayoendelea katika Taasisi hiyo. Hadi sasa jumla ya wagonjwa saba wamefanyiwa upasuaji kati ya hao watoto watano na watu wazima wawili.
Madaktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo na mishipa ya damu  kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia  wakiendelea na kazi ya kumfanyia  mgonjwa upasuaji wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting).

Picha na JKCI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad