HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 23 November 2017

NAIBU WAZIRI ULEGA AFANYA ZIARA KATIKA KISIWA CHA MAFIA

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amefanya ziara katika Kisiwa cha Mafia kwa ajili kukagua shughuli za uvuvi pamoja na kumuona Samaki aina Papa Potwe.
Akizungumza na Wavuvi , Watendaji wa Kisiwa hicho, Ulega amesema kuwa sekta ya Uvuvi inatakiwa ilete maendeleo ikiwa rasilimali hizo zitatumika ipasavyo.
Ulega ameiagiza  Halmashauri ya Mafia ndani ya siku saba kuhakikisha wavuvi wapate barafu kwa kuuziwa bei ya chini ili kuweza kupata mapato.
Amesema kuwa wananchi wa Mafia hawaelewi maana ya Hifadhi ambapo wanatakiwa kupewa elimu ili kuondokana na mgogoro wa hifadhi.
Ulega amesema Halmashauri  inashindwa kupata mapato ya kujiendesha kutokana  na kutokuwa wabunifu juu ya kutengeneza mapato ikiwa pamoja  kuwasumbua wananchi kwa vitu visivyo na mapato.
Aidha amesema kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuli amefuta ushuru kwa wafanyabiashara wanaochukua biashara kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Amesema kuwa hakuna sheria ndogo inayozidi sheria Mama juu ya Halmashauri Mafia kutunga sheria ndogo ya kuchukua ushuru wa mazao ya bahari yanayotoka wilaya moja kwenda nyingine wakati sheria hiyo ilishafutwa.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akiwa katika boti kuelekea katika kisiwa cha Mafia ikiwa ni ziara ya kuangalia shughuli za maendeleo ya Uvuvi katika kisiwa hicho ambacho kinategemea kipato chake kwa ajili ya mazao ya baharini .
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na wavuvi pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Mafia juu ya usimamizi wa shughuli za uvuvi ambazo zinafanyika katika kisiwa cha Mafia
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akikagua kiwanda cha uchakataji samaki kilichopo Mafia ambacho ni kiwanda cha uchakataji samaki kwa ajili ya usafirishaji .
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akipokea ripoti kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Shaib Ahmed Nnunduma (kulia) jinsi shughuli za Uvuvi zinazofanyika katika Kisiwa hicho .
 Watalii wakimuangalia samaki aina ya Papa Potwe ambaye anapatikana Tanzania kwa miezi mitano wakati sehemu nyingine anakaa miezi miwili.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii Mafia

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad