HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 28, 2017

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUDHULIA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS WA KENYA, MHE. UHURU KENYATTA JIJINI NAIROBI LEO

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akimpongeza Rais Uhuru Kenyatta kwa kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa awamu ya pili, katika Sherehe zilizofanyika leo kwenye uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi, Kenya. Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhulia sherehe hizo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia) akiwa pamoja na viongozi wengine wa nchi mbalimbali waliohudhulia katika Sherehe za kuapishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Rais Uhuru Kenyatta iliyofanyika leo kwenye uwanja wa Moi Kasarani Mjini Nairobi, Kenya. Mhe. Samia Suluhu Hassan amehudhulia sherehe hizo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad