HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 24 November 2017

KIJANA ANAYEDAIWA KUUA MTU ASIYEJULIKANA AFIKISHWA MAHAKAMANI

 Na Karama Kenyunko wa Blogu ya Jamii
Kijana wa miaka 22, anayeishi Ipililo Maswa mkoani Shinyanga leo Novemba 24, 2017 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kumuua mtu asiyejulikana.
 Kwa mujibu wa chanzo cha Habari cha uhakika kijàna huyo ambaye alikamatiwa katika kituo cha mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam na alikutwa akiwa na viungo vya binadamu ambavyo ni sehemu za mbalimbali za siri za mwanamke na nyara za serikali.
Mshtakiwa Nkonja amesomewa mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.
Wakili wa serikali Nassoro Katuga akisoma hati ya mashtaka amedai kati ya Oktoba Mosi na 30 mwaka huu katika eneo la Kahama Shinyanga na Kituo cha Mabasi cha Ubungo jijini Dar es Salaam, alimuua mtu ambaye bado hajafahamika.
Hata hivyo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Decemba 8, mwaka huu. Upelelezi bado haujakamilika

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad