HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 30 November 2017

DKT SHIKA KUTAMBULISHWA RASMI USIKU WA 900 ITAPENDEZA DAR LIVE MBAGALA

Dokta Louis Shika akiwa na meneja wake Catherine Kahabi wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna tamasha hilo la usiku wa 900 itapendeza zaidi litakavyokuwa siku hiyo na kuwataka watu kuhudhuria na kumsikiliza bilionea huyo atazungumza nii juu ya maisha yake kiujumla pale Dar live,leo katika ukumbi wa habari maelezo Jijini Dar es Salaam.

Na Agness Francis Blogu ya Jami.
Dokta Louis Shika ambaye ni mshindi wa mnada wa uuzaji wa Nyumba za Lugumi awakaribisha wakazi wa Jiji la Dar es Salaam kushiriki tamasha la usiku wa 900 itapendeza ambapo atazungumzia maisha yake kiujumla toka alipoanzia hadi mpaka sasa alipofikia.

Meneja wa Dkt Shika Catherine Kahabi amesema hayo leo Jijini Dar es salaam katika ukumbi wa habari maelezo ambapo Tamasha hilo limeandaliwa na udhamini wa Global tv ambapo mgeni rasmi atakuwa aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Rawrence Kego Masha.

Aidha amesema kuwa lengo ni kutaka kumtambulisha rasmi Dkt Shika ili kumuweka katika muonekano wa kibilionea na akiwa kama miongoni mwa watu walioshika umaarufu mkubwa kwa muda mfupi hapa nchini

Hata hivyo bilionea huyo amemalizia kwa kuwataka wakazi wa Dar es Salaam kuhudhuria Tamasha hilo ambalo litasindikizwa na Burudani mbalimbali ikiwemo wanamuziki na vikundi vya vichekesho hapa nchin.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad