HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 10 September 2017

LUGUMI APOTEZA NYUMBA YA KWANZA, MAGOROFA MAWILI YAKOSA WANUNUZI

Kampuni ya udalali ya YONO  imesimamia shuguli za kuuzwa kwa mnada gorofa lililopo upanga mali ya kampuni ya Lugumi Enterprises Limited na kununuliwa na kampuni ya Al-Naeen Enterprises kwa shilingi Milioni 700.

Mnada huo wa magorofa hayo na majengo mengine mawili  ambayo yamekosa wateja kutokana na bei zake kuwa juu ukilinganisha na ukubwa wa jengo bado hayajapatiwa wateja.

Akizungumza wakati wa mnada huo, Mkurugenzi wa kampuni ya YONO Scolastica Kevela amesema kuwa Nyumba ambazo zimekosa wateja zinauzwa Shilingi Milioni 460 na zinapatikana eneo la Mbweni JKT Wilaya ya Kinondondi jijini Dar es Salaam.

Kampuni ya Lugumi Enterprises Limited inahusishwa na kashfa ya ubadhirifu wa fedha za serikali pamoja na kudaiwa kodi na TRA masuala ambayo yamepelekea kuuzwa kwa majengo hayo na kulipia kodi TRA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad