HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 20, 2017

TUMESHAKABIDHI RIPOTI KWA UONGOZI, TUNASUBIRI MAJIBU TUANZE KAMBI - KOCHA MTIBWA

Kikosi cha Mtibwa.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

KOCHA msaidizi wa timu ya Mtibwa Zuberi Katwila amesema kuwa kwa sasa anasubiri maamuzi ya Mwenyekiti wa klabu hiyo baada ya kumkabidhi ripoti ya mwaka mzima ya kikosi hicho.

Akizugumza na Mtandao huu, Katwila amesema kuwa ameshakabidhi ripoti kwa Uongozi wa klabu hiyo  na wanatarajiwa kuanza maezoezi Julai mosi mwaka huu kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2017/18.

Katwila amesema, hawezi kuweka wazi ni wachezaji gani watakaoachwa ila ripoti nzima imeweka wazi wachezaji wanaohitajika kuachwa na sababu zao kwani kila mmoja amewekewa muda aliocheza na alicheza katika kiwango cha juu au chini.

"kila mchezaji ameainishwa katika ripoti katika vipengele tofauti kama aliweza kucheza kwa muda gani na kwa kiwango gani, mbali na hilo wapo ambao wameshindwa kuonyesha kiwango kikubwa na pia nao nimewaandikia sababu za kuachwa,"alisema Katwila.

Amesema, ukiachilia hilo pia katika ripoti yake ameweka wazi wachezaji anaowahitaji ila cha zaidi anasubiri majibu ya uongozi kuhusiana na wachezaji hao na iwapo watashindikana kupatikana hatua ya itakayofuata ni kuita wachezaji katika kufanya majaribio katika timu yao.

Katwila amesema mpaka sasa hawajajua ni wapi wataweka kambi hiyo ya maandalizi ya ligi hadi pale watakapopata maelekezo kutoka kwa Uongozi kama watakaa Manungu au nje ya mkoa wa Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad