HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 7, 2017

SHULE YA SEKONDARI BARABARA YA MWINYI SEKONDARI YAKARABATIWA

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Temeke, Eric Kilangwa (wa pili kulia) na Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick wakifurahia baada ya uzinduzi wa madarasa matano, ofisi ya walimu na eneo la makusanyiko baada ya kufanya ukarabati katika shule ya sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Pamoja nao ni Mwenyekiti wa shule hiyo, Sostenes Nyenyembe (kulia), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya Bam International Africa Noreen Mazalla (kushoto) na Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa.(Picha na Robert Okanda Blogspot). Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa akiwatembeza wageni kujionea ukamilishwaji wa mradi wa ukarabati wa madarasa na ujenzi wa eneo la makusanyiko kabla ya kufanya uzinduzi.

Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya Barabara ya Mwinyi alipotembelea mojawapo ya madarasa matano, kampuni hiyo iliyoyakarabati eneo la Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Emmentrudice Chilewa.

Wanafunzi wakiimba shairi la kuwashukuru viongozi wa kampuni hiyo.
Mgeni Rasmi, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Temeke, Eric Kilangwa (wa pili kulia) akimkabidhi cheti cha shukrani kwa Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick.

Waalimu na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bam International wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Barabara ya Mwinyi iliyopo Buza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla hiyo.
Mkurungezi wa Miradi wa Kampuni ya Bam International, Wolfgang Marschick na Meneja Maendeleo ya Biashara, Noreen Mazalla wakipanda mti wa ukumbusho katika eneo la makusanyiko la shule hiyo uliofanywa kampuni hiyo katika shule ya Barabara ya Mwinyi Buza jijini Dar es Salaam Juni 6 2017. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Eric Kilangwa (wa tatu kushoto) na Mwenyekiti wa shule hiyo Sostenes Nyenyembe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad