HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 12, 2017

RAUNDI YA PILI SPRITE BBALL KINGS YAENDELEA, MECHI NNE ZAPIGWA

Timu ya Mpira wa Kikapu ya Land Force.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MASHINDANO ya Sprite BBall Kings yameendelea tena jana kwa michezo minne kupigwa katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Airwing.



Ikiwa ni hatua ya pili ya mashindano hayo baada ya wiki iliyopita kupatikana kwa timu 18 zilizoingia baada ya kupigwa michezo takribani 26.

Mchezo wa kwanza uliwakutanisha timu za Dream Chaser na Land Force na timu ya Dream Chaser kuibuka na ushindi wa vikapu 92 dhidi ya 72 za Land Force.

Mechi ya pili iliwakutanisha Kurasini Heat ambaye alitoka na ushindi mnono wa vikapu 124 dhidi ya Bongo Hits aliyepata vikapu 14, The Fighters wakaumana na Chanika Legends na kufanikiwa kushinda kwa vikapu 93 dhidi ya vikapu 16.

Mechi ya mwisho iliwakutanisha TMT na God With Us na kuhitimisha mechi ya nne kwa TMT kuibuka na ushindi wa vikapu 72 dhidi ya 23 huku kukisubiriwa mechi zingine zitakazopigwa wiki ijayo kuwapata washindi wa jumla watakaoingia hatua ya tatu ya mashindano hayo.

Mratibu wa Mashindano hayo ya Sprite BBall Kings Basilisa Biseko amesema kuwa baada ya kumalizika kwa mechi za wiki ijayo timu zilizopata alama nyingi ndiyo zitafanikiwa kuingia hatua inayofuata.

"Timu zilizopata alama nyingi katika michezo ya leo na katika michezo ya wiki ijayo ndiyo watakaofanikiwa kuingia hatua inayofuata ya michuano ya Sprite BBall Kings,"amesema Basilisa.

Michuano hiyo inayodhaminiwa na Sprite kwa kushirikiana na East Africa Tv na Redio inaendelea tena wiki ijayo katika viwanja vya Chuo cha Bandari na mshindi kamili ataondoka na kitita cha shiling milion 15


Timu ya Land Force wakiumana na Dream Chaser katika mechi ya hatua ya pili ya mashindano ya Sprite Bball Kings jana katika Viwanja vya Airwing.
Timu ya Mpira wa Kikapu Dream Chaser.


Mchezaji wa Dream Chaser akifunga kwa mtindo wa kudanki katika mchezo wa hatua ya pili ya mashindano ya Sprite BBall Kings.                                                

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad