HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 21 June 2017

Mwanasheria ya TBS huru, akamatwa tena.

Na Karama Kenyunko blogu ya jamii


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemfutia kesi mwanasheria Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Baptister Marco Bitaho (54) baada ya upande wa mashtaka kuomba kufanya hivyo.

Bitaho alikuwa akikabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la kuishi na kufanya kazi nchini Tanzania bila kuwa na kibali. 

Mashtaka hayo yamefutwa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa baada ya Mwendesha Mashtaka kutoka Uhamiaji, Method Kagoma kuiomba mahakama imfutie mwanasheria huyo mashtaka yake chini ya kifungu cha 98(a)cha sharia ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA).

Hata hivyo baada ya mshtakiwa huyo kuachiwa huru alikamatwa tena na yupo katika Idara ya Uhamijai kwa ajili ya mahojiano. 

Mapema mwezi huu, ilidaiwa kuwa Mei 19,2017 huko Kinondoni katika ofisi ya uhamiaji, Bitaho akiwa raia wa Burundi alikutwa akiishi nchini bila ya kuwa na kibali.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo, Bitaho alikutwa akifanya kazi kama mwanasheria Mkuu wa TBS bila ya kuwa na kibali kinachomruhusu kufanya kazi hapa nchini.Iliongezwa kuwa, Julai 6 mwaka 2011 katika ofisi ya Uhamiaji ya Dar es Salaam iliyopo wilaya ya Ilala, mshtakiwa huyo akiwa raia wa Burundi alitoa taarifa za uongo kuhusu maelezo yake binafsi wakati akijaza fomu ya kuomba hati ya kusafiria namba CT (5)(Ai).

Ilidaiwa kuwa, kitendo hicho cha kutoa taarifa za uongo kilimuwezesha Bitaho kupata hati ya kusafiria ya Tanzania yenye namba AB 474856 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria za nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad