HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 20, 2017

MTOTO SHUKURU ARUHUSIWA MUHIMBILI, AFYA YAKE YAIMARIKA

Mtoto Shukuru Kisonga (16) ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) baada ya kupatiwa matibabu na afya yake kuimarika.
Mtoto Shukuru alifikishwa  katika  Hospitali ya Taifa Muhimbili Mei 16, mwaka huu akitokea Tunduru ambako aliripotiwa kuishi kwa kunywa mafuta , sukari na maziwa.
Baada ya kufikishwa MNH alifanyiwa uchunguzi na timu ya madaktari Bingwa  na kubaini kwamba ana ugonjwa wa Selimundu pamoja na upungufu wa madini ya chuma na kwamba upungufu wa madini hayo ulisababisha anywe mafuta, sukari na maziwa.
Kwa upande wake Mama mzazi wa mtoto Shukuru,  Mwanabibi Mtenje amesema amepata faraja kuona afya ya mtoto wake imeimarika na sasa anaweza kula chakula chochote.
“Kwakweli namshukuru Mungu, pia nawashukuru  sana madaktari na wauguzi wa Muhimbili  kwani  hali ya mwanangu ilikuwa mbaya, alikuwa hawezi kula chochote  zaidi ya kunywa mafuta, maziwa na sukari, lakini baada ya kupatiwa matibabu,  afya yake imeimarika na sasa anaweza kula vyakula vyote,’’ amesema Mama Shukuru.
Awali mtoto Shukuru  alipelekwa katika Hospitali ya Misheni Tunduru kwa ajili ya kupatiwa matibabu, lakini ugonjwa haukooneka na baadaye alipelekwa hospitali  Nyangao mkoani Lindi.
 Mtoto Shukuru Kisonga (16) akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alifikishwa Mei 16, 2017 kwa ajili ya kupatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa na Selimundu na upungufu wa madini chuma. Mtoto huyo sasa anaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu na madaktari wa hospitali hiyo.
Mtoto Shukuru Kisonga (16) ameruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambako alikuwa amelazwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa selimundu na upungufu wa madini chuma.  Kushoto ni mama yake Shukuru, Mwanabibi Ntenje.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad