HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 24, 2017

Kizimbani kwa kutapeli mahujaji

Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii

MKURUGENZI wa Kampuni ya Travel House Global, Sojan Varghese amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu tuhuma za kujipatia USD 88,012 kwa mahujaji. Imedaiwa kuwa, fedha hizo alipewa kwa ajili kuwakatia tiketi ya ndege mahujaji zaidi ya 119 wa Chama cha Karismatiki Katoliki Tanzania.

Varghese anadaiwa kuchukua fedha hizo kutoka kwa John Ngotty kwa ajili ya usafiri wa mahujaji hao waliokuwa wakitaka kusafiri kuelekea nchi za Roma, Italia  na Israeli kwa ajili ya hija.

Mwendesha mashtaka, wakili wa serikali, Adolph Mkini amedai Desemba 23, 2016 ofisi za Kampuni hiyo zilizopo mtaa wa Jamhuri, mshitakiwa alijipatia USD 7,012 kutoka kwa Ngotty fedha ambazo ni kwa ajili ya nauli ya kupata tiketi ya ndege kwa Wakarismatiki 119 kutoka Dar es Salaam kwenda Roma na Israeli. Desemba 23, mwaka jana mshitakiwa huyo alijipatia USD 9,500 kupitia hundi namba 000005 kutoka kwa Ngotty kwa ajili ya kuwakatia tiketi ya ndege.

Mbele ya Hakimu Mkazi,Wilbard Mashauri imedaiwa kuwa, Januari 11, Varghese alijipatia USD 9,500 kutoka kwa Ngotty kwa lengo la kutumika kununulia tiketi za ndege kwa mahujaji hao. Aidha mshtakiwa anadaiwa kujipatia USD 9,500 kwa hundi namba 000008 kutoka kwa Ngotty.

Januari 31, mwaka huu, Varghese alijipatia USD 37,500 kutoka kwa Ngotty na Aprili 12, pia alijipatia USD 15,000 kwa ajili ya nauli ya tiketi ya ndege kwa wanachama 199 wa Karismatiki. Mshitakiwa amekana mashitaka yote na amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Mahakama ilimtaka mshitakiwa kuwasilisha Sh milioni 100 au hati ya mali yenye thamani hiyo pamoja na wadhamini wawili wanaotambulika kisheria.

Pia alimtaka mshitakiwa kuwasilisha pasi yake ya kusafiria na kwamba haruhusiwi kutoka nje ya Mkoa wa Dar es Salaam. Kesi hiyo itatajwa tena Julai 6 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad