HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 4 April 2017

YALIYOJIRI LEO BUNGENI MJINI DODOMA BAADA YA VIKAO VYAKE KUANZA LEO

 Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Viwanja vya Bunge kwa ajili ya kushuhudia kiapo cha Mke wake Mama Salma Kiwete aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mbunge.
 Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akiwasili katika viwanja vya Bunge Mjini Dodoma kwa ajili ya kula kiapo na kuanza majukumu yake. 

 Rais Mstaafu wa awamu ya  nne, Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa kikao cha bunge mjini Dodoma Aprili 4, 2017. Mheshimiwa Kikwete alikwenda bungeni kushuhudia kuapishwa  kwa mkewe mama Salma .
 Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Salma Kikwete akisindikizwa na wabunge wanawake kwenda kula kiapo cha kutumikia kazi yake leo Bungeni Mjini Dodoma.
 Spika wa bunge, Job Ndugai akimwapisha Mama Salma Kikwete kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017.
 Mama Salma Kikwete akiapa kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza Mama Salma Kikwete baada ya kuapishwa kuwa mbunge, bungeni mjini Dodoma Aprili 4, 2017.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
 Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsi Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
 Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe. Ramo Makani akijibu hoja mbalimbaliz za wabunge katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 Mjini Dodoma.
 Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda Mama Tunu Pinda akisalimia wabunge mara baada ya kutambulishwa kati ya wageni wa Spika leo Bungeni Mjini Dodoma kushoto ni Mke wa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mama Devotha Gabriel.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge Kazi Ajira na Watu wenye Ulemevu Mhe. Jenista Mhagama akitengua kifungu cha Bunge kwa kuomba Bunge kuendesha shughuli zake siku ya Jumamosi na siku za kazi kuendelea kwa awamu ya pili  saa kumi jioni badala ya saa kumi na moja jioni. 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akifuatilia shughuli za Bunge leo Mjini Dodoma.

Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad