HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 11 April 2017

SERIKALI IMETEKETEZA VIFARANGA 67500 KWA KUTOFATA SHERIA.

Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvivu Mhe.William Ole Nasha

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA
Serikali imesema kuwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2017 vifaranga 67500 vilivyoingizwa nchini kinyume na sheria viliteketezwa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvivu Mhe.William Ole Nasha Bungeni Mjini Dodoma wakati wa Maswali na Majibu.

“Wako wawekezaji wachache  ambao hupewa vibali maalum vya  kuingiza mayai au vifaranga wa kuku wazazi (Parents Stock) tu,ukaguzi kwa ajili ya kudhibiti uingizaji vifaranga na mayai unaendelea na hatua kali zinachukuliwa kwa yeyote anayekamatwa kwa kukiuka utaratibu”,Alisisitiza Mhe.Ole Nasha.

Amesema kuwa  kuanzia mwaka 2006 serikali iliweka katazo la kuingiza kuku na mazao yake nchini ili kudhibiti ugonjwa hatari wa Mafua ya Ndege na hakuna mwekezaji yeyote aliyeruhusiwa kupewa kibali cha kuingiza vifaranga au mayai nchini kwa ajiri ya biashara.

Aidha amesisitiza kuwa Sheria ya Magonjwa ya Wanyama na .17 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2007 na 2010 zinatumika kudhibiti na kukagua uingizaji katika maeneo ya mpakani,bandarini na viwanja vya ndege.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad