HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 22 March 2017

YANGA YAWAONDOA HOFU MASHABIKI, WASEMA MC ALGER NI KAMA TIMU NYINGINE

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa 

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa wanashukuru wamepata ratiba kwa wakati ya hatua ya mtoano wa kombe la Shirikisho na mechi ya kwanza wanaanzia hapa nyumbani dhidi ya wapinzani wao MC Alger toka Algeria. 

Akizungumzia hilo, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema kuwa hawana hofu na MC Alger kwani ni kama timu nyingine na kikubwa zaidi amewaondoa hofu mashabiki na kuwataka watulie kwani benchi la ufundi linaendelea kukinoa kikosi kwa ajili ya maandalizi.

" Yanga SC ni timu kongwe na bora na tumejipanga kupata matokeo nyumbani na ugenini. Tumezungumza na wachezaji wetu pamoja na benchi la ufundi kujiandaa vyema kimbinu , kiufundi na kisaikolojia kushinda mchezo huu. Mechi kama hizi unapopata ushindi mzuri wa nyumbani , basi unapunguza mlima wa kuupanda ugenini,"amesema Mkwasa.

Mkwasa amesema kuwa MC Alger ni timu nzuri na amekuwa bingwa wa Afrika hivyo kila mtu atataka kuiona na sisi tunawaheshimu kwa historia yao lakini tunakwenda kupambana kutafuta ushindi na zaidi ameweka wazi msisitizo kuwa hivi karibuni wame

"muda ukifika tutawajuza wapi mechi itafanyikia kama ni hapa jijini au popote Tanzania. Kwa sasa bado hatujaamua lolote katika hilo hivyo uwanja wa taifa unabaki kutambulika kama uwanja wa nyumbani." 

Mkwasa akizungumzia sapoti ya mashabiki katika mchezo wao , alieleza kinagaubaga jinsi gani klabu inahitaji sapoti yao mwanzo mwisho , " mashabiki na wadau wote wa soka nchini tunawaomba kuipa sapoti timu yetu muda wote wa dakika 90 itakapokuwa uwanjani.

"tunawafahamu vyema wenzetu kwa fitina zao hususani mechi za kwao . Mara nyingi huzipanga usiku ili wapate fursa ya kuwasha miale yao na vitochi kuumiza macho ya wachezaji . Tunawaandaa wachezaji wetu katika hali zote pia umakini wa kuripoti kila tukio kwa mamlaka husika . " alimaliza katibu mkuu huyo wa Yanga SC ndugu Charles Mkwasa. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad