HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 20 March 2017

YANGA KUANZA KUJIFUA KESHO, KUSUBIRI DROO YA CAFNa Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BAADA ya kurejea kutoka nchini Zambia kwenye mchezo wa  kombe la Klabu Bingwa Afrika na kuondolewa kwenye michuano hiyo, kikosi cha Yanga kinatarajiwa kesho kuanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya ligi kuu Vodacom.

Yanga waliiondolewa kwenye michuano hiyo na kurejea kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo kesho kutakuwa na  droo ya kupanga timu za kucheza hatua ya mtoano ya 32 na timu 16 kuingia makundi.

Droo hiyo itapangwa kesho na michezo inatarajiwa kuanza kuchezwa Aprili 7 hadi 9 na atakayefanikiwa kushinda ataingia hatua ya makundi ya 16 bora.

Akizungumza na Globu ya Jamii, Meneja wa timu ya Yanga Hafidh Saleh amesema kuwa kesho kikosi kitaanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya ligi na mivhuano mingine kwani hawatakuwa na muda wa kupoteza.

"sisi  kama benchi la ufundi tunachofahamu ni kuwa tunaendelea na mazoezi kama kawaida lakini kuhusiana na mechi ya kirafiki na timu ya Polisi Dodoma ni suala la utawala labda umuulize katibu mkuu Charles Mkwasa," amesema Saleh baada ya kumuuliza kuhusiana na mechi ya kirafiki na Polisi Dodoma iliyopangwa kuchezwa Machi 25.

Kwa sasa akili zetu zote ni kukipa muda kikosi kiweze kupata muda wa klupumzika na kujipanga kwa michezo inayofuata kwani wachezaji waliobaki ni wengi kuliko wale walioenda kwenye timu zao za Taifa kujumuika nao, saleh aliweka wazi msimamo wa benchi la ufundi.

Hizi ndio timu zinazoweza kukutana na Yanga

1. Maghreb Fez - MOROCCO
2. Zesco - ZAMBIA
3. Al Masry - MISRI
4. Rayon Sports - RWANDA
5. JS Kabyile - ALGERIA
6. Plantinum Star - S. AFRICA
7. Recretivo Libolo - ANGOLA
8. Asec Mimosas - IVORY COAST
9. Smouha - MISRI
10. MC Alger - ALGERIA
11. CS Sfaxien - TUNISIA
12. Mbabane Swallows - SWAZILLAND
13. Club African - TUNISIA
14. Ittihad Thanger -  MOROCCO
15. Supersport United - S. AFRICA
16. Hillal Obayed - Sudan


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad