HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 21 March 2017

Watanzania wazidi kunufaika na M-Bet

Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, James Mbalwe(kushoto) mshindi wa shilingi milioni 125/- Mkazi wa mkoa wa Pwani, Victor Byarugaba(katikati)wakimsikiliza kwa makini Msemaji wa M bet,Godluck Wambura akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ya kumkabidhi mshindi huyo hundi yake mwishoni mwa wiki alizojishindia kupitia mchezo wa kubahatisha Supper 12 unaoendeshwa na M-bet. 
 
Na Mwandishi wetu
Watanzania wengi nchini waendelea kunufaika na matokeo ya kubashiri mechi kupitia Kampuni ya M-bet na kujishindia Shilingi Milioni 125/-.

Akiongea na mtandao huu mwishoni mwa wiki katika hafla fupi ya kukabidhiwa hundi yake iliyofanyika jijini Dar es Salaam,Victoria Byarugaba(30)Mkazi wa Mkoa wa Pwani amewashauri watanzania wote wenye umri unaoruhusiwa kisheria kujitokeza kubashiri matokeo ya mechi mbalimbali kupitia Kampuni ya M-Bet .

"Nashukuru sana M-Bet kwa kuniwezesha kujikwamua kimaisha, nitatumia fedha hizi kutimiza ndoto zangu ingawaje nimeajiriwa na moja ya kampuni za mawasiliano lakini nilikuwa na ndoto kubwa ya kununua kiwanja na kuanza ujenzi natumai ndoto hii imetimia sasa", alisema Byarugaba.

Kwa upande wake, Msemaji wa M bet,Godluck Wambura alisema kuwa Victoria alifanikiwa kuzoa kitita hicho baada ya kufanikiwa kutabiri mchezo wa Super 12 kwa mtindo wa kucheza kawaida. “Tunafarijika kumkabidhi Victoria kitita hicho cha Sh milioni 125/- akiwa ndiye mtanzania wa kwanza kujishindia kitita hichi kupitia m-Bet,” alisema Wambura.
Mkazi wa mkoa wa Pwani, Victor Byarugaba(kushoto)akikabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 125/- na Msemaji wa M bet,Godluck Wambura(kulia) alizojishindia kupitia mchezo wa kubahatisha wa supper 12 unaoendeshwa na kampuni hiyo,anayeshuhudia katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, James Mbalwe.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Sheria wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, James Mbalwe(watatu kushoto)akiwa kwenye picha ya pamoja na Mshindi wa shilingi milioni 125/- Mkazi wa mkoa wa Pwani, Victor Byarugaba, Meneja wa huduma kwa wateja wa M-bet,Jaykishan Kaba(kushoto)pamoja na Msemaji wa M bet,Godluck Wambura wakati wa hafla fupi yakumkabidhi hundi mshindi huyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alizojishindia kupitia mchezo wa kubahatisha Supper 12 unaoendeshwa na M-bet.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad