HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 21 March 2017

STARS YAINGIA KAMBINI LEO, SAMATTA, FARID KUINGIA NCHINI USIKU WA LEO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Mshambuliaji na Nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samatta anatarajiwa kuwasili nchini leo kuanzia Saa 4:00 usiku kujiunga na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mchezo ya kirafiki ya kimataifa wiki ijayo.

Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi mbili, kwanza na Botswana Machi 25 na baadaye Burundi Machi 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na pamoja na Samatta, mchezaji mwingine wa Tanzania anayecheza Ulaya, Farid Mussa anatarajiwa pia kuwasili leo.

Wakati Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji atatua kwa ndege ya Shirika la Uturuki Saa 4:00 usiku, Farid wa DC Tenerife anatarajiwa kutua kuanzia 9:00 Alfajiri kwa ndege ya KLM.Taifa Stars itamkosa mchezaji mwingine wa Ulaya, Thomas Ulimwengu wa AFC Eskilstuna ya Sweden, ambaye hayuko fiti.

Taifa Stars inaingia kambini leo kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam na kikosi hicho cha kocha Salum Mayanga aki

saidiwa  na kocha wa Makipa, Patrick Mwangata, Meneja wa timu Danny Msangi, Mtunza Vifaa Ally Ruvu wakati Daktari wa timu atakuwa Richard Yomba na Daktari wa viungo akiwa ni Gilbert Kigadya.Nyota wengine walioitwa Taifa Stars ni walinda milango
Aishi Manula (Azam FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja 
Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).

Walinzi wa kati ni 
Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).

Viungo ni 
Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya (Simba SC), 

Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC)

Wakati washambuliaji ni 
Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yussuf (Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu Shooting).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad