HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 21 March 2017

RC PWANI AHIMIZA KILIMO KINACHOSTAHIMILI UKAME ILI KUJIEPUSHA NA BAA LA NJAA

Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo akikagua mashamba ya mihogo kijiji cha Mbwara wilayani Rufiji katika ziara yake mkoani humo kuhimiza kilimo cha mazao yanayostahimili ukame. (picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi, Rufiji

MKUU wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo, amehimiza kupanda mazao yanayostahimili ukame na kukomaa haraka ikiwa ni sanjali na muhogo, mtama, viazi vitamu na kunde. Amesema wakati mvua zikiendelea kunyesha haina budi watu wakalima mazao hayo ili kujiepusha na baa la njaa ambalo huwa likijitokeza katika baadhi ya maeneo.

Mhandisi Ndikilo, ameeleza hayo katika ziara yake aliyoianza mkoani hapo kutembelea wilaya sita kujionea hali ya mazao mbalimbali ya Kilimo na kuhamasisha Kilimo. "Kipindi hiki hali ya hewa sio nzuri sana na utabiri wa hali ya hewa ulitabiri hakutokuwa na mvua za vuli za kutosha na ilitokea". "Na za masika zinavyoonekana zitakuwa chini ya wastani hivyo tusipojipanga na Kilimo na kutokuwa waangalifu tutatumbukia kwenye njaa "alisema mhandisi Ndikilo.
Mhandisi Ndikilo alisisitiza kulima mazao yanayostahimili ukame ili kuwa na chakula cha kutosha. Hata hivyo, aliambiwa na wakazi wa Mbwara wilayani Rufiji kuwa mihogo wanalima lakini tatizo ni wanyama kama ngedere, nguruwe ambao wanaharibu na kula mazao.

Mkuu huyo wa mkoa wa Pwani alisema, watumie maafisa maliasili wilaya kwa kuandika barua maalum kwa Mkurugenzi wa halmashauri na wataalam watakwenda kutatua tatizo hilo. Mhandisi Ndikilo akiwa wilaya ya Rufiji, alikagua ghala jipya la Ikwiriri AMCOS ,kukagua mashamba ya mihogo kijiji cha Mbwara.

Pia alitembelea mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu Mbwara sekondari na kuzungumza na waandishi. Mhandisi Ndikilo ameendelea na ziara yake wilaya ya Kibiti na march 22 atakuwa Mkuranga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad