HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 20, 2017

MOTO WA PETROL WASABABISHA VIFO VYA WATU WATATU PEMBA

Mamia ya wananchi leo wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Micheweni Abeid Juma Ali na Afisa Mdhamini afisi ya Makamu wa pili wa rais Pemba, Ali Salim Mata kwenye mazishi ya watu watatu wa familia moja, akiwemo mtoto wa miaka sita, waliofariki kutokana na nyumba yao kuteketea kwa moto, uliosababishwa na mafuta ya petroli shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni Pemba
Vitu vilivyoungua na kusalimika kwa moto vya marehemu Makame Omar Mata (60) baada ya nyumba yake kuteketea kwa moto na watu watatu akiwemo mtoto wa miaka sita walifariki shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
Nyumba ya marehemu Makame Omar Mata (60), ilioteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watu watatu, akiwemo baba, mama na mtoto wa miaka sita, ajali hiyo iliotokezea shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, ilitokana na mafuta ya petroli.

Baadhi ya vitu vilivyoungua na kusalimika kwa moto vya marehemu Makame Omar Mata (60) baada ya nyumba yake kuteketea kwa moto na watu watatu akiwemo mtoto wa miaka sita walifariki shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba.
Makame (25) alieungua moto, kwenye ajali ya moto uliotokezea ndani ya nyumba yao na kuuwa watu watatu, akiwa kwenye hospitali ya Micheweni akipatiwa matibabu, baada ya nyumba yao kuteketea yote, moto huo ulisababishwa na mafuta ya petroli.
Omar Makame Omar (19), alisalimika na kuungua kwa moto, ulioteketeza nyumba yao na mama yake, ndugu yake wa miaka sita na baba yake mzazi kufariki, kutokana na kuripuka kwa mafuta ya petrol, shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni Pemba.
Sheha wa shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni Rahma Mohamed Shaame akizungumza na waandishi wa habari, juu ya tukio la kufariki watu watatu kwenye shehia yake, baada ya nyumba yao kuungua moto, iliosababishwa na mafuta ya petroli.
Nyumba ya marehemu Makame Omar Mata (60), ilioteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watu watatu, akiwemo baba, mama na mtoto wa miaka sita, ajali hiyo iliotokezea shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, ilitokana na mafuta ya petroli.
Mamia ya wananchi wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Micheweni Abeid Juma Ali na Afisa Mdhamini afisi ya Makamu wa pili wa rais Pemba, Ali Salim Mata kwenye mazishi ya watu watatu wa familia moja, akiwemo mtoto wa miaka sita, waliofariki kutokana na nyumba yao kuteketea kwa moto, uliosababishwa na mafuta ya petroli, shehia ya Shumba mjini wilaya ya Micheweni Pemba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad