Na Humphrey
Shao, Globu ya jamii
Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam imelitaka shirika la Nyumba nchini (NHC) kuheshimu amri ya
mahakama na kuondoa notisi walizowapa wakazi wa Keko mpaka kesi ya msingi
itakapoisha.
Jaji
Beatrice Mutungi wa mahakama hiyo amewaonya NHC leo baada ya wakili wa
wapangaji wa magorofa ya Keko yaliyopo barabara ya uwanja wa taifa jijini,
Daniel Lisanga kuwasilisha maombi ya kupinga wateja wake kuhamishwa.
Katika maombi
hayo, Wakili Lisanga anapinga kitendo cha NHC kupeleka notisi ya siku 14 kwa
wateja wake akitaka wahame katika nyumba hizo kabla kesi ya msingi waliyofungua
haijaisha.
Akiongea
mahakamani hapo, wakili Lisanga amesema kuwa Februari 27, mwaka huu wakati shauri
hilo la ardhi lenye namba 23 likiendelea kusikilizwa, kwa makusudi na huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha
sheria NHC Ilipeleka notisi ya siku 14 kwa wapangaji hao ikiwataka wahame.
Hata hivyo,
NHC wameidharau amri ya mahakama iliyotolewa na Jaji Augustine Shangwa, Oktoba
6, mwaka juzi iliyowataka kutowabugudhi wapangaji hao mpaka kesi ya msingi
itakapoisha.
NHC
wanadaiwa kuwatumia Ubapa Auction Mart kwenda kuwaondoa wapangaji hao ambao ni
jumla ya familia 60 zinazoishi katika block C,F,G na H.
Akizungumza nje
ya mahakama wakili Lisanga amesema kuwa madai ya msingi ya shauri hilo bado yako
mahakamani hivyo wamesikitishwa sana na kitendo cha kudhalilishwa kwa wateja
wake kinachoendeshwa na NHC.
“Idara ya
mahakama ni muhimili na inastahili kuheshimiwa na mtu yoyote ambaye yupo chini
ya sheria”, amesema.
Hata hivyo mahakama haikuweza kuendelea na
shauri hilo leo baada ya wakili wa NHC, Aloyce Sekule kushindwa kufika
mahakamani
Wakili Daniel Lisanga, akizungumza na wapangaji wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC), mara baad aya kutoka mahakama ku jijini Dar es Salaam
Wapangaji wa Shirika la nyumba la Taifa (NHC),wakitoka nje ya mahakama kuu Tanzania.
No comments:
Post a Comment