HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 23 March 2017

LAPF YAANZA KUSAJILI WANACHAMA WAPYA WA SEKTA BINAFSI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mfuko wa Pensheni wa LAPF umeanza kuandikisha wanachama kutoka sekta na serikalini za binafsi na ongezeko hilo imetokana na wanachama kutumia fursa ya kuchagua mfuko ulio sahihi wenye ubora .

Akizungumza leo na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja Mafao wa LAPF , Ramadhani Mkeyenge amesema pamoja na kuwepo kwa huduma hiyo mfuko umeboresha huduma za ulipaji wa mafao kwa wakati.

‘’ Mwanachama wa LAPF anaekaribia kustaafu hutaarifiwa mapema ili kujiandaa kwa kuwa na nyaraka zote zinazohitajika na hulipwa siku moja kabla ya kustaafu’’.

Mkeyenge ameongeza kuwa kwa mwaka 2015\2016 mfuko wa Pensheni umeweza kulipa kiasi cha milioni 107 kwa wanachama wake huku kipindi cha mwaka 2011\2012 mfuko ulifanikiwa kulipa kiasi cha milioni 38.1 kwa wanachama hii ilitokana na ongezeko la wanachama.

‘’Mwaka 2015\2016 wanachama 316 wamepewa mikopo kiasi cha milioni 10.5 ambapo hadi kufikia sasa LAPF ina wanachama zaidi ya 165,000’’.aliongeza Mkeyenge.

Mfuko wa Pensheni umekuwa ukiwahudumia wanachama wake kwa takribani zaidi ya miaka 70 na mafao ambayo yanatolewa ni pamoja na pensheni ya uzee,warithi,ulemavu,mikopo ya elimu pamoja na pensheni ya kujitoa.
Meneja Mafao wa LAPF , Ramadhani Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya LAPF inavyofanya kazi kwa wanachama leo jijini Dar es Salaam,kulia ni Afisa Matekelezo Mwandamizi LAPF, Katiti Katiti. Picha na Emmanuel Mssaka, Globu ya jamii.
Afisa Matekelezo Mwandamizi LAPF, Katiti Katiti akizungumza na waandishi wa habari juu ya LAPF inavyofanya kazi kwa wanachama wake, leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mafao wa LAPF , Ramadhani Mkeyenge
Baadhi ya Wanahabari wakifuatilia mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad