HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 21 March 2017

KITUO CHA UTALII MKOANI MBEYA CHAHAMASISHA UTALII WA NDANI KWA MBIO ZA BAISKELI

KITUO cha Utalii Mkoani Mbeya (Uyole Cultural Tourism Enterprises) wakishirikiana Chama cha Baiskeli Mkoa wa Mbeya (MBECA) pamoja na Elimisha za Jijini Mbeya wamefanikisha safari ya Kilomita 240 kutoka Mbeya mjini mpaka Wilayani Kyela kwa kutumia usafiri wa baiskeli kwa mafanikio makubwa.

Msafara huo wenye lengo la kutangaza Utalii wa ndani na kuhamasisha mchezo wa mbio za Baiskeli nchini ulifanikiwa kufika salama wilayani humo na kuweka kambi katika hoteli ya Ngonga Beach Resort iliyopo Kilomita 15 kutoka Kyela Mjini, Aidha, msafara huo ulitembelea pia mpakani mwa Tanzania na Malawi kwenye Mji wa Kasumulu ili kujionea shughuli mbalimbali zinavyofanyika ndani ya mpaka huo.

Akizungumza wakati wa kuupokea msafara huo, Afisa Utalii wa Wilaya ya Kyela, James Mbaga aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Claudia Kitta, alisema kuwa wameupokea ugeni huo kwa mapokezi mazuri, ambapo waliwapeleka kunako kivutio kimoja wapo cha Utalii kwenye Daraja la Kiteputepu ili wameze kujionea Kivutio hicho, kwani daraja kama hilo ni adimu kuonekana maeneo mengine nchini Tanzania.

Msafara huo ulioongozwa na Waratibu wa Uyole C.T.E, Amos Mwamugobole, Debora Kallomo na Modesto Mwalingo huku waendesha baiskeli wakiambatana na Makamu mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Mbeya, Rasi Kaise pamoja na Mhazini wa chama Mkoa, Lucas Mhagama kama waangalizi wa mbio hizo (Race Officials). Picha zote na Fadhil Atick a.k.a MrPengo.
Waendesha baiskeli mkoani Mbeya wakiendelea na safari yao kutokea Jijini Mbeya kwenda Kyela umbali wa kilometa 240 ukiwa ni msafara wa kuhamasisha utalii nchini na pia kuihamasisha jamii kufanya mazoezi hasa ya kutumia Baiskeli.

Mratibu kutoka Uyole cultural tourism Enterprises, Amos Asajile mwamugobile akizungumza jambo na waendesha baskeli Pamoja na uongozi WA Ngonga Beach Resort Mara baaya ya kufika wilayani kwela katika Hotel ya Ngonga Beach.
Sehemu ya waendesha Baiskeli waliosafiri kutokea Mbeya mpaka Kyela umbali wa kilometa 240.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad