HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 21 March 2017

Kesi Madai ya CUF kutajwa mwezi ujao

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Wanachama nane wa chama cha CUF, akiwemo mbunge wa Jimbo la Kaliua Tabora, Magdalena Sakaya leo wamewasilisha pingamizi la awali dhidi ya kesi ya madai iliyofunguliwa na bodi ya wadhamini ya  CUF

Pingamizi hilo la awali limewasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa wadaiwa, Mashaka Ngole na litasikilizwa Mbele ya Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri.
Katika pingamizi hilo, wakili  Ngole amedai kuwa, maombi  yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Bodi ya wadhamini ya CUF kupitia Wakili Hashimu Mziray hayawezi kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Amedai kuwa maombi hayo yanashughulikiwa  katika maombi namba 23 ya 2016 yaliyopo Mahakama Kuu Masijala ya Dar es Salaam.

Ngole ameendelea kudai kuwa,  muombaji hana mguu wa kusimamia (mamlaka) ya kufungua kesi dhidi ya wajibu maombi na kwamba maombi hayo hayana msingi  kwa sababu yameshindwa kubainisha jina  la mwandishi wa masula ya fedha. Aidha wameomba mahakama itupilie mbali maombi hayo kwa garama.

Kufuatia pingamizi hilo, wakili Mziray aliiomba mahakama iwapatie muda wa kujibu pingamizi hilo kwa kuwa  walikwisha patiwa nakala ya pingamizi hilo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 12 mwaka huu ambapo mahakama itasikiliza pingamizi hilo. Kesi ya msingi imepangwa kutajwa Mei 8,2017.

Awali, Bodi ya wadhamini ya CUF, kupitia wakili Mziray ilifungua kesi ya madai mahakamani hapo ikiomba  zuio la muda ili Sakaya na wenzake saba wasiweze kujihusisha na uongozi wa chama na kufanya mikutano na waliwasilisha maombi hayo chini ya hati ya dharura.

Katika maombi hayo iliyofunguliwa chini ya hati ya dharula, wajibu maombi ni  Magdalena Sakaya na wenzake Thomas Malima, Maftah Nachumu, Omar Masoud, Abdul Kambaya, Salama Masoud, Zainabu Mndolwa na Jafari Mneke.

Katika maombi ya  bodi ya wadhamini wanaiomba  mahakama itoe zuio la muda kwa kuwazuia wajibu maombi ama  mawakala wao au watu wao kujihusisha katika masuala yoyote ya uongozi ama kufanya mikutano ya chama hicho, hadi maombi yatakaposikilizwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad