HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 22, 2017

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE YA ULINZI NA USALAMA YAKAGUA MRADI WA UJENZI -OFISI ZA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu (wa kwanza kushoto), akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo baada ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya, akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama (hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi wa ujenzi ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa ofisi za jeshi hilo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi huo  leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Adadi Rjabu na anayefuatia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama,Kapteni Mstaafu George Mkuchika, akichangia hoja wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua ujenzi wa ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dar es Salaam leo.

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad