HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 22 March 2017

JUKWAA LA WAHARIRI LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MAKONDA

 Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena (katikati) akizungumza katika mkutano ana waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu tamko la vyombo vya habari la kususia kuandika habari za matukio ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambaye ijumaa iliyopita alivamia kituo cha Clouds Media usiku akiwa na askari waliokuwa na bunduki. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Dar Press Club, Shadrack Sagati na Mjumbe wa TEF, Lillian Timbuka.PICHA NA RICHARD MWAIKENDA
 Meena ambaye alisoma  tamko la pamoja la TEF, Dare sSalaam Press Club na Umoja wa Vilabu vya Habari nchini akijibu moja ya maswali ya wanahabari.

Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) leo  limevitaka vyombo vya habari nchini kutokuandika au kutangaza habari zozote zinazomhusisha Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam, Paul Makonda.

TEF wameyasema hayo leo katika  taarifa yao na kulaani vikali kitendo cha Makonda cha kuvamia kituo cha Utangazaji cha Clouds usiku wa Machi 17 akiwa na askari wenye silaha.

“Kwa mantiki hiyo, tunamtangaza Ndugu Paul Makonda kuwa ni Adui wa Uhuru wa Habari, na yeyote yule atakayeshirikiana naye katika kukandamiza uhuru wa habari nchini,” ilisema taarifa hiyo ya TEF iliyoandikwa na Mwenyekiti wake, Theophil Makunga.
 Wanahabari wakiwa kazini


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad