Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice
Singano Mallya (katikati) akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati
wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando
itakayowawezesha
wateja wake kuongea bila kikomo. Wa (pili kushoto) ni Mkurugenzi wa
Masoko wa Airtel, Isack Nchunda na wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini
(kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako
Wasanii wa kundi la Weusi, Joe Makini
(kulia) , Niki wa Pili (katikati) na Gnako wakitumbuiza jijini Dar es
Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ya Airtel ijulikanayo kama
Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja Airtel kuongea bila kikomo.
Mkurugenzi wa
Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano Mallya (katikati) akisisitiza
jambo wakati wa uzinduzi wa Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando
itakayowawezesha wateja wake kuongea bila kikomo
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice
Singano Mallya (wa pili kushoto) na wasanii wa kundi la Weusi, Joe
Makini (kulia), Niki wa Pili(wa pili kulia) na Gnako kwa pamoja
wakizindua
Ofa kabambe ijulikanayo kama Hatupimi Bando itakayowawezesha wateja
wake kuongea bila kikomo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel,
Isack Nchunda.
Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua OFA kabambe
ijulikanayo kama HATUPIMI Bando itakayowawezesha wateja wake wote
nchini kuongea bila kikomo mara tu baada ya kujiunga.
“Airtel
HATUPIMI Bando” itapatikana katika vifurushi mbalimbali ikiwemo
kifurushi cha siku, wiki na mwezi vilivyosheheni dakika zisiso na
kikomo zinazowawezesha wateja wa Airtel kuongea na kufanya mengi zaidi
bila kuwa na wasiwasi wa kuishiwa muda wa maongezi kwa kuwa hakuna
kupimiwa dakika za maongezi.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa ofa
hii kabambe, Mkurugenzi wa Masoko, Isack Nchunda alisema “ Airtel
Hatupimi, sasa Hatupimi dakika zenu za maongezi, tunaleta huduma hizi
nafuu kwa kuwa tunaamini katika kuendelea kuboresha huduma zetu ili
kukidhi mahitaji ya wateja wetu kwa kuwapatia thamani ya pesa zao
katika huduma na bidhaa zetu.
“HATUPIMI Bando” itawapatia
wateja wetu nchi nzima uhuru wa kuongea na familia, marafiki na wadau wa
biashara zao kulingana na aina ya kifurushi mteja alichochagua ikiwemo
kifurushi cha siku, wiki na mwezi bila kujali vifurushi vyao kuisha muda
wa maongezi. Kuna vifurushi vya Hatupimi kwa siku vya hadi shilingi
1000/= pia vipo vya wiki kwa shilingi 5000, na vilevile unaweza kujiunga
na HATUPIMI kwa mwezi kwa shilingi 10,000/= ili ufurahie huduma
yakutopimiwa dakika zako ongea bila kikomo
Airtel tunaamini
“HATUPIMI” ni ofa ya kipekee sokoni, tunatoa wito kwa wateja wetu na
wateja wapya kujiunga sasa na kufurahia ofa hii kabambe inayowapa uhuru
wakuonge watakavyo bila kikomo. Aliongeza Nchunda
Kujiunga na
ofa ya HATUPIMI Bando piga *149*99# kisha chagua 1 kupata HATUPIMI kisha
chagua bando ya Siku, Wiki, Mwezi kulingana na mahitaji yako “
alisisitiza Nchunda.
Airtel imekuja na ofa yake ya HATUPIMI
ikiwa ni siku chache tu baada ya kuzindua ofa kabambe kupitia huduma ya
Airtel Money, Vile vile airtel wiki hii ilizindua kampeni ya kufungua
maduka yake 2,000 yatakayotoa huduma kwa wateja ili kuwafikishia wateja
wake wote huduma zao popote walipo.
No comments:
Post a Comment