Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
MKURUGENZI wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Silvia Temu amesema kuwawanafunzi wanaohitimu wanatakiwa kwenda kufanya kazi kwa juhudi kubwa na kutokuacha kujiendeleza na kujifunza kwani dunia inabadilika na magonjwa yanazidi kujitokeza kila siku.
Aliyasema hayo, wakati wa kongamano la Mjasiri lililowakutanisha wanafunzi waliosoma zamani katika Chuo Kikuu cha Afya, Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na wanafunzi wanaohitimu na kuwataka kuendelea na utafiti wa magonjwa mbalimbali yanayowazunguka jamii.
Prof
Temu amesema kuwa MUHAS wameweza kufanya kitu kizuri sana kwa
kuwakutanisha wanafunzi waliomaliza hapa na mkusanyiko huu utasaidia
kuweza kuleta mawazo mapya na zaidi yatasaidia kwenye kukuza na
kuendeleza sekta ya afya.
"kwa
niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako,
tunaoenda kuwapongeza sana MUHAS kwa jitihada nzuri waliyofanya ya
kuwakutanisha pamoja wanafunzi waliosoma miaka ya nyuma pamoja na hawa
wanaohitimu katika ngazi mbalimbali kwani tunachokijua ni kuwa
watabadilishana uwezo hasa kwa wale waliokuwa washapata uzoefu wa muda
mrefu,"amesema Prof Temu.
Makamu
Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof. Ephata Kaaya amesema kuwa kongamano hili
la Majasiri litaleta manufaa makubwa sana kwani kutawawezesha wanafunzi
wanaohitimu na waliomaliza miaka ya nyuma kufanya kazi kwa pamoja,
kwani Majasiri wanachangia kwa kiwango kikubwa katika Chuo kwa kutoa
mawazo na hata fedha kwa ajili ya kuendeleza maendeleo ya chuo.
Kaaya
amesema kuna changamoto nyingi sana katika kuendeleza maendeleo ya
chuo hususani kwa upande wa fedha ila kwa kuwakutanisha hawa Majasiri
kutasaidia kwa namna moja au nyingine kwenye kutatua matatizo ya chuo
cha MUHAS.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Silvia Temu akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako wakati wa Kongamano la Majasiri wa Chuo Kikuu cha Afya, Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Silvia Temu (katikati)akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kutoka kushoto ni
Makamu
Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof. Ephata Kaaya, Mwenyekiti wa kamati ya Chuo Mariam Joy Mwaffisi, kutoka kulia ni makamu mwenyekiti wa kongamano Dr Ellen Senkoro na Mwenyekiti wa wa kongamano hilo Prof Charles Mgone. Waliosimama ni wahitimu na watumishi wa MUHAS.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Silvia Temu akiangalia baadhi ya maonesho yaliyoandaliwa na Wahitimu wanaomaliza kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) leo Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Silvia Temu akiwa na Makamu
Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof. Ephata Kaaya (kushoto), Mwenyekiti wa wa kongamano la Majasiri wa Chuo hicho Charles Mgone.
Baadhi ya wahitimu na wahitimu wakiwa makini kufuatilia kongamano hilo. Picha zote na Zainab Nyamka.
No comments:
Post a Comment