HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 22, 2016

WASOMI WATAKIWA KUWA WABUNIFU KATIKA KUPATA AJIRA

 . Mjumbe wa kamati ya maandalizi  wa mkutano huo, Thea Mtau, akimkaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar , Mwajuma Pembe.
 Waziri wa Elimu na  mafunzo ya amali wa serikali ya Mapindzu Zanzibar, Mwajuma Pembe akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo.

Baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu wakisikiliza kwa makini wakati wa kufunga kongamano hilo
 Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar , Mwajuma Pembe akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kongamano hilo


Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
IMELEZWA Kuwa bado kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa ajira kwa wahitimu ya mafunzo ya elimu ya juu licha ya kuwepo kwa vyuo vya kutosha nchini.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa mafunzo ya ufundi na Amali wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar, Mwajuma Pembe alipokuwa akifunga kongamano la siku mbili la wasomi na wakufunzi wa vyuo vikuu nchini jijini Dar es Salaam.

“Bado kuna changamoto kubwa sana licha ya kuwepo kwa wahitimu wa elimu ya juu kila mwaka hali inayotokana na upungufu wa viwanda hapa nchini hivyo ndio maana serikali ya awamu ya tano inasisitiza uchumi wa viwanda hili kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira hapa nchini”amesema Waziri Pembe.

Waziri huyo ametoa wito kwa wasomi na wahitimu wote hapa nchini kuwa wabunifu katika kila jambo wanalosomea hili kuweza kujikwamua kiuchumi na kutumia elimu waliyonayo katika mazingira yanayowazunguka.

Alimaliza kwa kusema kuwa wanazuoni wanatakiwa kuja na majibu muafaka ambayo yatawezesha wahitimu kujikwamua kiuchumi kwa kuweza kujiajiri katika masuala mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad