HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 22, 2016

SERIKALI KUHIFADHI TAKWIMU ZA URITHI WA UTAMADUNI USIOSHIKIKA KWA VIZAZI VIJAVYO

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati)  akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha kuhusu urithi wa Utamaduni Usioshikika inayoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa wadau wa utamaduni leo Jijini Dar es Salaam. Wakwanza kushoto ni Mtaalam wa  Utamaduni wa UNESCO Bi. Rehema Sudi anayefuatia ni Mtaalam wa Mipango kutoka UNESCO Bw. Mathias Luhanya na wakwanza kulia ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Bibi. Deirdre Solani
 Mtaalam wa Mipango kutoka UNESCO Bw. Mathias Luhanya (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha kuhusu urithi wa Utamaduni Usioshikika kwa wadau wa utamaduni  iliyoratibiwa na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Mtaalam wa  Utamaduni wa UNESCO Bi. Rehema Sudi.
Mtaalam wa Mipango kutoka UNESCO Bw. Mathias Luhanya (katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha kuhusu urithi wa Utamaduni Usioshikika kwa wadau wa utamaduni  iliyoratibiwa na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni(UNESCO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Mtaalam wa  Utamaduni wa UNESCO Bi. Rehema Sudi.

Na: Genofeva Matemu
Serikali imeahidi  kuhifadhi  kumbukumbu na takwimu sahihi za urithi wa Utamaduni usioshikika kwa lengo la kuuendeleza na kuiwezesha jamii kuulinda kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokua akifungua warsha ya siku kumi iliyoandaliwa na  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kuhusu urithi wa Utamaduni Usioshikika  leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa warsha hiyo Prof. Gabriel amewataka washiriki kujifunza vizuri ili baadaye waweze kusaidia  katika kuwekeza, kuibua, kutambua na kutunza urithi wa utamaduni ushioshikika kwani hiyo ndio njia mojawapo  itakayowavutia watalii wengi kuja nchini  kujifunza tamaduni zetu zisizoshikika.
“Utamaduni ni nta inayowaweka watu pamoja, ni vyema mafunzo haya na utaalamu mtakayoipata izingatie kuibua fursa na kutambua tamaduni ambazo hazishikiki kwani serikali ina malengo na matumaini makubwa sana kutoka kwenu” alisema Prof. Gabriel.
Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Utamaduni kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Lily Beleko amesema kuwa Tanzania iliweka saini na kuridhia mkataba wa kulinda urithi wa utamaduni usioshikika ambao ulipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzaia mnamo mwaka 2011.
Anaongeza kuwa  baadaye  UNESCO kwa kushirikiana na Wizara inayohusika na mambo ya Utamaduni wamekua  wakishirikiana katika kutoa  mafunzo kwa wadau wa utamaduni na watu binafsi  kuhusu namna ya kuhifadhi urithi  wa utamaduni usishikika  ambapo mafunzo hayo yanafanyika kwa   mara ya nne sasa  huku  lengo likiwa ni  kutekeleza mkataba huo.
Aidha Bibi. Beleko amesema kuwa watanzania wengi wamekua wakidhani kuwa utamaduni ushioshikika unahusiana na mambo ya kichawi  hivyo kutotilia maanani umuhimu wake kitu ambacho si kweli kabisa kwa kuwa maana halisi ya  utamaduni usioshikika  unahusisha vitu vinavyohusiana na mazingira, maendeleo ya watu pamoja na mila na desturi zao yakiwemo maongezi, nyimbo, maigizo, midundo ndani ya ngoma ambayo yanaambatana na ala.
Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bw. Mathias Luhanya amesema kuwa dhumuni la warsha ni pamoja na kuwajengea uwezo wadau wa utamaduni namna ya kuhifadhi urithi wa utamaduni usioshikika ili baadaye waweze kuorodhesha urithi huo kwani Tanzania ina bahati ya kuwa na jamii zaidi ya 120 hivyo ni matarajio kuwa urithi wa utamaduni usioshikika umesheheni ndani ya kila jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad