Mtaa Kwa Mtaa Blog

MKUU WA WILAYA YA ILALA SOPHIA MJEMA APOKEA MALALAMIKO YA MGOGORO WA MAENEO YA VIWANJA ENEO LA PUGU KINYAMWEZI.


Wananchi waliokuwa na mashamba na nyumba katika eneo la Pugu kinyawezi leo wamewasilisha malalamiko yao mbele ya Mhe. Sophia Mjema ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala. 
Malalamiko hayo yanatokana na kuwepo kwa sintofahamu za hatma ya maeneo yao ambayo yamechukuliwa na mamlaka ya uendelezaji wa viwanja vya ndege. Wananchi hao kutoka katika Mitaa ya Kipunguni, Kigilagila na Kinyamwezi hawajalipwa fidia kama ilivyokuwa imedaiwa kupitia mradi wa upimaji wa Viwanja katika eneo hilo. 
Wakizungumza katika Mkutano huo uliotishwa na Mkuu wa Wilaya kwenye viwanja vya  na kuhoji uhalali wa mradi huo. Ofisi ya AfisaTarafa ya Ukonga ilielezwa kuwa, kuanzia mwaka 2001 hadi 2006 Mamlaka ya Viwanja vya ndege ilifanya uthmini wa maeneo mbalimbali ya wenyeji wenye mashamba katika maeneo ya mitaa ya Kata za Pugu, Majohe  na Mitaa ya Viwege, Kinyamwezi, Zavala, Mgeule na Taliani. 
Bw, Awadhi Mtani akimkabidhi Mkuu wa Wilaya Ramani za Mipaka za eneo mradi ambazo ni chanzo cha mgogoro unaoendelea. 
Hadi sasa ahadi zilizotolewa kuhusiana na malipo ya fidia hayajafanyika na pia hawajapewa viwanja vyao na hali ikiwa mashamba yao yamekwishachukuliwa. Sintofahamu hiyo imesababisha Wananchi wengi kukosa Imani ya Serikali yao. Miongoni mwa wananchi hao wapo waliopokea fedha ambazo hazilingani na thamani ya maeneo yao ambayo yameshachuliwa na pia hazitoshelezi kumalizia  ujenzi na kuwapelekea kuishi kwenye nyumba za kupanga.
Mkuu wa wilaya akisikiliza malalamiko ya wakazi wenye wenye malalamiko ya viwanja na nyumba eneo la pugu kinyawezi
Aidha wakilalamika mbele ya Mhe. Sophia wananchi hao wamewalaumu baadhi ya viongozi wanaosiamia mradi huo kwa kutowapatia taarifa sahihi za mradi huo hali ambayo imesaabisha kuwepo kwa migogoro baina ya wakazi hao hali inayotishia usalama wa Maisha miongoni mwao. 
‘’Mhe Mkuu wa Wilaya tunaomba kupewa viwanja vyetu’’ walidai wananchi hao  
Akizungumza kwa uchungu mbele ya Mkuu wa Wilaya Bibi Gaudensia Paskali alieleza kuwa wakati wa zoezi hilo nyumba zake tatu zilibomolewa na alipofuatilia alipewa majibu ya kuwa kwakuwa nyumba zake ni za udongo hastahili kulipwa fidia.  
Aliendelea kueleza kuwa alifuatilia suala hili hadi kwa aliyewahi kuwa WAZIRI WA Ardhi Anna Tibaijuka ambaye hakuwaki kukuonana naye hadi leo hajafahamu hatma yake. Akiwa ni Mwanamke mjane hali hiyo imemsababishia mgogoro na watoto wake wakimtuhumu kuuza eneo hilo. 
Katika kubainisha mapungufu zaidi katika mradi huo baadhi ya wananchi walilalamikia kupewa maeneo mbadala ambayo haiendani ya matumizi yaliyokusudiw wapo waliopewa maeneo mbadala ambayo ni eneo la makaburi na siyo makazi.
“Mheshimiwa Tunaishi Maisha magumu, hatujui hatma yetu tunaomba utusaidie” 
Mpima Ardhi wa Manispaa ya Ilala Bw. Ramadhani Chamwiti akitoa ufafanuzi mbele ya Wananchi wa Mitaa ya Kipawa, Kigilagila na Kinyamwezi katika Mkutano huo.
Mheshimiwa Mhe. Boniventure Mphuru Diwani wa Kata ya Pugu akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Wananchi walioshiriki kwenye Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala  uliofanyika leo 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala   aunda Timu ya watu wanne kutoka miongoni mwa Wanachi waliokuwa na malalamiko itakayoungana na wataalam kutoka Halmashauri  na Ofisi yake kufuatilia Majibu ya Wizara ya Ardhi  kuhusiana na malipo ya Fidia baada ya maelezo ya Mhandisi wa TAA kuwa na utata. 
 Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akizungumza na Wananchi wa Pugu kinyawezi  juu ya kuunda Timu ya watu wanne kutoka miongoni mwa Wanachi waliokuwa na malalamiko watakaoungana na wataalam kutoka Halmashauri  na Ofisi yake kufuatilia malipo na Fidia baada ya maelezo ya Mhandisi wa TAA kuwa majibu ya utata leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala,Edward Mpogolo na akitoa ufafanuzi wa baadhi ya maswali yaliyoulizwa na Wananchi walioshiriki kwenye Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akipokea nyaraka  mbalimbali kutoka kwa,Awadhi Mtani  katika Mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akikagua maandalizi  barabaraa Lumumba itakayo tumika na Wafanyabiashara wadogowadogo (Machinga) kila siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. Leo jijini Dar es Salaam.akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa Ndg. Msongela Palela, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni. na Katibu Tawala wa Wilala ya Ilala Edward Mpogolo
.Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akisisitiza jambo mara baada ya kukagua maandalizi ya barabara ya Lumumba kutumika na Wafanyabiashara wadogowadogo (Machinga) kila siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili  leo (kushoto)ni ni Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget