HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 15, 2016

MADEREVA BODABODA WAWALAMIKIA ASKARI WA VODAFASTA

Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Arusha David Mwakiposa akiwa anaongea na waendesha bodaboda wa wilaya ya Arusha
  Waendesha bodaboda wakiwa wanamsikiliza katibu tawala wa wilaya kwa makini

 Na Woinde Shizza, Arusha 


Baadhi ya Vijana wa mkoa wa Arusha wanaofanya kazi ya kuendesha bodaboda wamelalamikia kitendo cha polisi wajulikanao kwa jina la Voda fasta kuwatoza rushwa kila kona pamoja na jiji kutowapa mikopo ya Vikundi jambo ambalo wamedai linawanyima raha na uhuru wa kufanya kazi . 

Hayo wamesema leo wakati mkutano baina yao na katibu tawala wa Wilaya ya Arusha Arusha David Mwakiposa wakati alipokutana nao kusikiliza kero zao zinazowakabili vijana hao ambao wanaendesha bodaboda 

Mbali na kero hiyo pia wameilalamikia Halmashauri ya jiji la Arusha kwa kushindwa kuwapa mikopo ambayo inaweza kuwasaidia kujiajiri wenyewe . 

Mmoja wa vijana hao bodaboda ambae alijitambulisha kwa jina la Daudi Molel alisema kuwa wamekuwa wakipata kero sana haswa kutoka kwa hawa askari polisi wanaojulikana kwa jina la Vodafasta kwani wamekuwa wakiwakamata hovyo na wamekuwa wakiwatafutia makosa mengi ili mradi tu wapewe rushwa. 

“uanajua unakuta mimi nimeshusha abiria gafla wanakuja anaanza kukutafutia makosa kibao ukikataa wanachomoa fungua wanaondoka nazokitu ambacho sio kizuri kabisa na akirithishi kabisa ,mimi nimeajiriwa tajiri amenituma fedha naitaji kupitia hiii hii bodaboda yangu nilishe familia nivalishe sasa jamani wanavyotudai rushwa kila mahali wanapotukamata wanatuhumiza sana tunaomba serikali itusaidie kwa hili “Alisema Asea Akyooo




Aidha aliongeza kuwa kwa upande wa jiji wamekuwa wanatoa fedha za mikopo kwa kificho sana kwani wamekuwa wanatoa fedha hizo kwa upandeleo na wanachagua vijana wa kuwapa na wao kama maderea bodaboda wamesahaulika kabisa hivyo wanauomba uongozi usika wawafikirie na wao ili waweze kupata mikopo kwa ajili ya kujinunulia pikipiki zao binafsi na waweze kujiajiri. 

Akijibu hoja hizo katibu tawala wa wilaya ya Arusha David Makiposa aliwasihi vijana hao kuunda vikindi na serikali ya wilaya ya Arusha ipo tayari kuwasimamia kuhakikisha nao wananufaika na pesa za mikopo ya jiji na serikali imeshatoa maelekezo kwa uongozi wa jiji kuhakikisha katika fedha watakazotoa kwa awamu hii wahakikishe kundi la boda boda linapewa kipaumbele cha kipekee. 

Alisema kuwa dhamira ya dhati ya serikali ni kutatua kero za wananchi kwa haraka iwezekanavyo ,hivyo azma ya serikali ya awamu ya tano ni kila kiongozi ama mtendaji anatatakiwa kutatua kero zilizopo katika eneo lake ipasavyo ivyo hana sababu ya kukaa ofsisini wakati kuna maelfu ya wananchi wanyonge wanateseka mtaani na wakiwa wanakabiliwa na kero mbalimbalimbali. 

Pia alitumia muda huo kuwashukuru watendaji wa kata kwa akuanza kutatua kero za wandesha bodaboda hao na kuwaagiza wengine kwenda kuweka program maalumu za kukaa na bodaboda na kuwasaidia shida zao na aliaidi kuendelea kuwafatilia. 

Aidha katika mambo ambayo kikao hicho kiliazimia ni pamoja na kuundwa uongozi wa wilaya kila kata ,kanda ya wilaya ndani ya siku saba ili waendesha bodaboda wapate chombo cha kuwasemea matatizo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad