Mtaa Kwa Mtaa Blog

C-Park Sound yatikisa Dar

Na MwandishiWetu
 Bendi ya muziki wa dansi ya C-Park Sound ya Kinondoni, Dar es Salaam imeendelea kutawala anga la muziki huo vitongoji vyote vya jiji ambapo mwishoni mwa wiki iliyopita ilidhihirisha kuwa ni moto wa kuotea mbali.

Jumamosi iliyopita, katika baa maarufu ya C-Park (zamani Matema) gazeti hili, lilishuhudia mamia ya mashabiki wakiburudika na muziki wa bendi hiyo huku wakisifu na kupiga makofi mara kwa mara kutokana na kuguswa mitima yao.

“Bendi hii kiboko, yaani siamini watu wote hawa wanaifuata bendi hii tu, au kuna promosheni hapa? Sio rahisi baa kujaza watu hivi wakati leo kumbi maarufu za Kinondoni nyingi ziko tupu. Kwa kweli nimewavulia kofia hawa vijana wa C-Park Sound,” akasema mpenzi mmoja anayejiita Lukaku.

Kiongozi wa bendi hiyo, Magazine, ameliambia gazeti hili kuwa, kujaza watu, kushangiliwa sana na kutuzwa pesa na zawadi nyingine ni kitu cha kawaida kabisa kwa bendi yake kwa hiyo hashangazwi na matukio ya aina hiyo.

“Tunajua nini tunafanya. Kila wiki tuko hapa baa ya C-Park, Kinondoni B, tunapiga muziki aina zote, tena kwa ubora wa asilimia mia moja. Hatubahatishi, kila anayekuja hapa huja tena na tena,” akajinasibu Magazine. 


Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget