HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 22, 2016

Airtel yaja na “WADATISHE INTANETI’ OFA kufaidisha wateja wake msimu wa sikukuu

Meneja Mawasiliano na Nembo wa Airtel, Bwn Arnold Madale, (kulia) pamoja na Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando na Meneja wa huduma za Intaneti Bw, Erick Daniel wakionyesha bango la offa mpya ijulikanayo kama “Wadatishe” ” itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata ofa kambambe ya Intaneti pamoja na vifaa nafuu vinayotumia intaneti kwa gharama nafuu zaidi wakati huu wa msimu wa sikukuu
Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya “Wadatishe Intaneti” itakayowawezesha wateja wa Airtel kupata ofa kambambe ya Intaneti pamoja na vifaa nafuu vinayotumia intaneti kwa gharama nafuu zaidi wakati huu wa msimu wa sikukuu. Wakishuhudia (kushoto) Meneja wa huduma za Intaneti Bw, Erick Daniel na kulia ni Meneja mawasiliano na Nembo, Arnold Madale. 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua Kampeni ya “Wadatishe Intaneti”  yenye OFA kabambe maalum kwa wateja wake nchi nzima ili waweze kufurahia huduma bora za Intaneti pamoja na kujipatia vifaa nafuu vinayotumia intaneti kwa matumizi binafsi au kwa kuwanunulia zawadi ndugu jamaa na marafiki katika msimu huu wa sikukuu.

Akiongea wakati wa Uzinduzi Wadatishe Intaneti OFA Meneja wa huduma za Intaneti Bw, Erick Daniel alisema  “Wadaitishe Intaneti” ni ofa ya kipekee kwa kuwa inatoa uhuru kwa kila mteja  kujichagulia kifurushi nafuu kinachoendana na kifaa anachotumia. Vipo vifurushi vya “Wadatishe Intaneti kwa siku, Wiki au Mwezi vya gharama nufaa ya hadi shilingi 500 kwa kupiga *149*99# na kuchagua Yatosha Intaneti. 

Vilevile mteja ataweza kujichangulia  Wadatishe intaneti OFA  nyingine kabambe kwa kupitia huduma ya Airtel Money kwa kupiga *150*60#  na kuchagua ofa kabambe kisha  Wadatishe Intaneti ambapo kwa shilingi 1000 tu utapata GB 1 ya intaneti na kwa shilingi 2000 tu pia utaweza kupata GB 2.5 papo hapo na kuanza kufurahia intaneti bora ya Airtel”.

Kwa kuongezea, Mteja yeyote ukienda na kununua kifaa chochote kinachotumia intanent kama vile simu za smartiphone, Modem za maajabu wingle, au home Wi-FI katika duka lolote la Airtel nchini utafaidi pia ofa ya punguzo bei la hadi shilling 79,000 na utaunganishwa na OFA ya intaneti kwa miezi 6 kuanzia sasa” alisema Erick.

Kwa Upande wake Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alisema “Airtel tunaendelea na  dhamira yetu ya kuhudumia wateja wetu kwa kuwapa kipaumbele kwa kila huduma yetu, hii ndio sababu kubwa inayotufanya tuwape wateja wetu nchini Uhuru mkubwa wa kujichagulia, kuanzia leo kupitia ofa za ‘Wadatishe intaneti’  tunaamini zitatoa unafuu mkubwa kwa  kuwaunganisha  ndugu, rafiki,  na familia kuwasiliana katika msimu huu wa sikukuu”.

Ofa zetu mwaka huu zinatoa punguzo kubwa sana kwa vifaa vinavyotumia Intaneti kama vile Home Wi-Fi  sasa utaipata kwa shilingi 79,000 tu badala ya shilingi 200,000 na utapewa Home Wi-Fi yako hiyo ikiwa na kifurushi cha GB 40 BURE. Kwa watakaonunua simu kama Magnus Z11 itaipata kwa shilling 79,000 tu ikiwa na ofa ya GB 12 kwa muda wa miezi 6. 

Vilevile kwa kupitia ushirika wetu na wadau wetu Techno na Huawei katika maduka yetu simu zao zote zitauzwa kwa bei za punguzo nafuu zaidi ya ilivyozoeleka.  Pia ili kukuongeze furaha kwa ofa tunazotoa kwa watumiaji wa Airtel msimu huu wa sikukuu utafaidi pia ofa mbalimbali za SMS za bure au muda wa maongezi wa ndani na nje ya mtandao” alieleza Nchunda.

Tunawahimiza wateja wetu kutembelea maduka yetu yote ya Airtel nchi nzima ili kujinunulia vifaa origino vya intaneti na kujiunganisha na huduma yetu bora kabisa ya Intaneti  kwa kupiga *149*99# na kuchagua Yatosha Intaneti ili kufurahia Wadatishe Intaneti Ofa” alimalizia kwa Kusema Bw, Mmbando.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad