Mtaa Kwa Mtaa Blog

WATOTO EXPO YAFANYIKA JIJINI DAR, WENGI WAVUTIWA NAYO

Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, Kampuni ya SS Brand International imeandaa Maonyesho ya Watoto yenye lengo kuhamasisha na kutangaza bidhaa, huduma na miradi ya watoto ili kukuza na kutoa upendeleo unaohitajika kuweza kuhamasisha utumiaji wa bidhaa bora za watoto.

Akizungumza katika kilele cha tamasha hilo la siku tatu lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa SS Brand International, Batul Adam amesema, tamasha hilo liliweza kuvutia watu mbalimbali ikiwemo wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali za watoto, wanahabari na familia ambao waliweza kujipatia taarifa kuhusu bidhaa na huduma za watoto zinazotolewa na makampuni hayo.

Huduma mbalimbali ziliweza kupatikana ikiwamo huduma ya bima ya Afya ya mtoto kutoka NHIF yaani Toto Afya, huduma za upimaji wa macho bure uliofanywa na kampuni ya Internatioal Eye Hospital, huduma zingine za bima kwa watoto, bidhaa za watoto na wakubwa na bidhaa nyingine, maelezo ya afya kutoka kwa wataalam n.k

Watoto wadogo waliopelekwa na wazazi wao katika maonyesho hayo, waliweza kushiriki mashindano ya kutambaa kwa wale wa kati ya umri wa kuanzia miezi mitano mpaka kumi na mbili ambayo yalidhaminiwa na bidhaa ya Softcare ya Sunda International na mshindi kujipatia diapers za kutumia miezi sita.

Maonyesho hayo yalidhaminiwa na kampuni ya Dar Fresh na Afiya, NHIF, Sundal International, PEPSI, MITAN.

Mashindano hayo yanategemea kufanyika tena baada ya miezi sita ambapo inatarajiwa makampuni mengi zaidi yataweza kushiriki na kuweza kutoa huduma na taarifa kuhusu bidhaa zao ipasavyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa SS Brand Internnational, Batul Adam akizungumza na Michuzi Tv kuhusu tamasha la maonyesho ya watoto katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Watoto waliofika kwenye tamasha hilo wakecheza michezo mbalimbali leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wazazi na walezi waliowate Watoto kwenye tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget