Mtaa Kwa Mtaa Blog

PICHA MBALIMBALI KATIKA TAMASHA LA MCHEZO WA SOKA 'KANDANDA DAY 2016' ZOTE ZIMEWEKWA HAPA

TIMU ya soka ‘Team Ismail’ imefanikiwa kuwagaragaza wapinzani wao wa jadi 'Team Dizo Moja' kwa kipigo cha mabao 4-1, katika tamasha la Kandanda day, lililofanyika Jumamosi katika Viwanja vya Jakaya M Kikwete Youth Park.

Kipigo hicho kwa 'Team Dizo', ni mfululizo wa matokeo mazuri ya Team Ismail,ambayo mwaka huu imeonekana kulipiza kisasi cha kuchapwa idadi hiyo ya mabao kama walivyofanya Team Dizo katika msimu wa mwaka 2014.

Mabao ya Team Ismail,yaliwekwa kimiani na Freddy Pastor aliyeweka kimiani mabao mawili,huku Gerald Bernald na Noah Katepa wakifunga bao moja moja na lile la kufutia machozi kwa timu Dizo likifungwa na mchezaji wao waliyemchukua kwa mkopo toka timu Ismail Wilfred Kadege.

Mwaka jana katika tamasha hilo, Timu Ismail,iliwatandika wapinzani wao kwa mabao 2 kwa mtungi,jambo ambalo mwaka huu liliongeza upinzani mkubwa ndani na nje ya uwanja kutoka kwa mashabiki wa timu hizo mbili.

Mbali na mtanange huo,mechi nyingine iliyovuta hisia za mashabiki waliohudhuria tamasha hilo ni mchezo wa fainali ya makundi ulizokutanisha timu za Dar City Fc na Coca Cola,ambapo katika mchezo huo, Coca waliigaragaza Dar City kwa mabo 3 kwa bila.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati,Patrick Dumulinyi,aliwashukuru wadhamini wote pamoja na timu shiriki kwa kufanikisha lengo la tamasha la mwaka huu lililobeba kauli mbiu ya Mpira na Dawati kufana kwa kiasi kikubwa.

“Ningependa kuwashukuru wadhamini wetu na timu shiriki,kwa kuungana kutimiza ndoto zetu za mwaka huu za kuisaidia jamii kwa kukusanya fedha za madawati,ambayo kabla ya kuisha kwa mwezi huu tunatarajia kuyakabidhi katika shule husika,”alisema Dumulinyi.


Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget