HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 25, 2016

MTANGAZAJI PJ ABURUZWA MAHAKAMANI NA EFM REDIO

Mtangazaji maarufu aliyewahi kutangaza kituo cha redio cha clouds fm nakujiunga na efm redio na baadaye kurudi tena clouds fm amefunguliwa mashtaka katika mahakama ya kazi Jijini Dar es salaam na efm redio kwa kile kinachodaiwa kuwa amekiuka mkataba wa kazi wa kituo hicho.

Kufuatiamashtaka hayo, Efm inadai fidia ya shilingi milioni 200 kwa mtangazaji huyo ambaye alijiunga na kituo hicho kutoka clouds fm na baadae akakatisha mkataba kiholela na kurudi tena clouds fm bila kufuata makubaliano pamoja na sheria alizokubaliana nazo katika mkataba wake pale alipojiunga na efm redio.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tarehe 23/11/2016 katika mahakama ya kazi Jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad