Mtaa Kwa Mtaa Blog

MAHAFARI YA SHULE YA MSINGI YA HERITAGE ENGLISH MEDIUM SCHOOL JINSI YALIVYOFANA JIJINI DAR LEO.

MAHAFARI ya tisa ya Wanafunzi wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) jinsi ilivyofana jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela, Mkuu wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School), Kebaso Elia akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule hiyo wakati wa mahafari ya tisa ya Darasa la Saba katika shule hiyo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) wakiwa katika mahafari ya tisa ya shule hiyo.
  Wanafunzi wa Shule ya English Medium ya Heritage iliyopo Banana Ukonga jijini Dar es Salaam wa wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wakati wa mahafari ya wanafunzi wa shule hiyo wanaohitimu masomo yao ya Darasa la Saba katika shule hiyo.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Mahafari ya tisa ya  Darasa la Saba katika shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) mara baada ya kutembelea maonesho ya masomo mbalimbali ya wanafunzi hao.
Amewapongeza walimu wa shule hiyo kwa kuwafundisha watoto hao hasa watoto wa darasa la awali katika shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) hasa katika taaluma pamoja na kuwafundisha watoto hao kuwa na hofu ya Mungu.

Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano ikiwa na sera ya Kusimamia na Kuimarisha elimu katika shule za awali katika shule zote za msingi kuwa na elimu ya awali hii itawezesha kutoa watoto wakiwa na uelewa bora.

Amesema katika Manispaa ya Ilala ina shule msingi za serikali 121, Shule za Binafsi za msingi 89 na shule za awali za serikali 99 pamoja na shule za binafsi za awali 84.
 Mwalimu Mkuu wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School), Kebaso Elia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa mahafari ya tisa ya Darasa la Saba katika shule hiyo.
Amewaomba Wizara ya elimu, sayansi na Teknologia iwapitishe waandishi wa vitabu vya kiada na ziada  ili kusitokee mkanganyiko katika ufundishaji wa watoto na kuwa na utofauti kati ya vitabu.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela atemelea maonesho ya masomo mbalimbali ya wanafunzi wa shule ya Mchepuo wa Kiingeleza katika mafahari ya tisa ya shule ya Heritage jijini Dar es Salaam.


 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela alipotembelea banda la maonesho ya Hisabati katika shule ya Heritage jijini Dar es Salaam leo.


 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela alipotembelea banda la maonesho ya masomo ya Darasa la awali na watoto wakionesha umahiri wao katika shule ya Heritage jijini Dar es Salaam leo.


 Kikundi cha Ngoma za asili cha shule ya Heritage.

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela alipotembelea banda la maonesho ya Masomo ya Sayansi katika shule ya Heritage jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) wakiwa katika mahafari ya tisa ya shule hiyo.


 Wahitimu wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) wakiingia ukumbini jijini Dar es Salaam leo katika mhafari ya tisa ya shule hiyo.
Baadhi ya waalimu wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) wakiwasindikiza wahitimu katika ukumbi wakati wa mahafari.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela akiingia katika eneo mahafari yanapofanyika akisindikizwa na Wanafunzi wa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) jijini Dar es Salaam leo.

  Baadhi ya wanafunzi mashujaa wa shule hiyo.
 Meza kuu.
 Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Wapiga ngoma wa kikundi cha Bendi  ya shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Heritage (Heritage English Medium School) wakiwa katika mahafari ya tisa ya shule hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget