HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, September 1, 2016

TUKIO LA KUPATWA KWA JUA LEO

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Kanali Mstaafu Chiku Galawa pamoja na Meneja Mawasiliano wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) , Pascal Shelutete pamoja na wananchi wengine wakiangalia tukio la kupatwa kwa Jua kutumia vifaa maalum muda huu, katika eneo la Mpunga Relini, Mbarali mkoani Mbeya. Tukio hilo limeonekana vizuri zaidi katika eneo hilo kuliko maeneo mengine nchini. Watu kutoka maeneo mbalimbali ya Dunia wako katika eneo hilo, kushuhudia kwa uzuri tukio la kupatwa kwa Jua.
Hivi ndivyo jua lilivyoanza kuonekana baada ya kupatwa, Hapo ni eneo la Mpunga Relini, Mbarali mkoani Mbeya, eneo lililotengwa kwa ajili ya kutizamia tukio hilo kwa uzuri zaidi.
 Wananchi wa Rujewa na Maeneo mengine mengi wakiwa eneo la tukio.
Na hata kina sie huku Mjini Dar es salaam tumelishuhudia tukio, japo tulitandwa na wingu zito. ila si haba tumebadatika kuiona kwa namna hii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad