HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, September 3, 2016

SUPER GIRLS BINGWA AIRTEL RISING STARS LINDI

Wachezaji wa timu ya Super Girls wakishangalia ubingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Lindi baada ya kuifunga VC Vito Malaika 4-1 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea Hadja Sekibo akikagua timu wakati wa fainali za michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Lindi zilizofanyika kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea. Super Girls ilishinda 4-1 dhidi ya VC Vito Malaika.
 Nahodha wa timu ya Super Girls Tatu Makota akipokea kombe la ubingwa wa michuano ya Airtel Rising Stars mkoa wa Lindi kutoka kwa Katibu Tawala wa wilaya ya Nachingwea Hadja Sekibo baada ya kuifunga VC Vito Malaika 4-1 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Nachingwea.

TIMU ya wasichana ya Super Girls imetwaa ubingwa wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars Mkoa wa Lindi baada ya kuichapa FC Vito Malaika 4-1 katika fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Katika michuano hiyo, Mpiruka Queens iliweza kuibuka mshindi wa tatu baada ya kuifunga Kipara Queens 2-1.

Katika mchezo wa fainali, Super Girls walianza kwa kasi na kuliandama lango la wapinzani wao tangu dakika za mwanzo lakini ilibidi kusuburi hadi dakika ya 15 ili kuandika goli la kwanza. Goli hilo lilofungwa kwa ustadi na mchezaji Ashura Mfaume baada kungongeana vizuri na Tatu Makota. 

Baada ya bao hilo, Super Girls waliendelea kutandaza kandanda safi na kufanikiwa kufunga bao la pili dakika ya 18 lilifungwa tena na Ashura Mfaume baada ya kuwalamba chenga mabeki watatu wa FC Vito Malaika. Bao la tatu lilifungwa na Alia Fikiri mnamo dakika ya 22 baada ya mabeki wa FC Vito kushindwa kuokoa mpira wa kona.

Timu ya FC Vito Malaika walipata bao lao pekee katika dakika ya 27 baada ya mchezaji Sarah Isaac kuachia shuti kali na mpira kujaa moja kwa moja wavuni. Hadi mapumziko, Super Girls 3 FC Vito Malaika 1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikasaka bao lakini ilikuwa ni Super Girls waliopata goli dakika ya 63 baada ya mchezaji Tatu Makota kufunga kwa penati baada ya beki wa FC Vito Malaika kunawa mpira kwenye eneo ya hatari.

 Akiongea kwenye fainali wa michuano hiyo,mgeni rasmi Hadja Sekibo ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa wa Nachingwea aliwapongeza kampuni ya Airtel kwa kuwekeza kwenye soka la wanawake nchini. ‘Nachukua nafasi ya kuwapongeza wenzetu wa Airtel kwa kuona umuhimu wa kuwekeza kwenye soka vijana wetu sana sana kwa wasichana. 

Tunatambua soka ni ajira, lakini kuwapa hawa vijana wetu wa kike nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, mnawafungulia milango ya kuonekana nchini nzima na pia kunawafanya kutoweza kujiingiza kwenye makundi yenye malengo mabaya kwani muda wao wa ziada wanatumia kucheza mpira. Kwa hivyo wanapongeza kwa kuweza kuunga mkono jitihada za serikali za kuwawezesha vijana kujiajiri’, alisema Sekibo.

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoani Lindi Ally Mkadeba alisema michuano ya Airtel Rising Stars imewawezesha kupanua wingo wa kutafuta vipaji vya soka mkoani na kufikia maeneo mengi ambayo bila Airtel Rising Stars wasingeweza kufika. Mkadeba aliongeza kuwa wakati wa michuano hiyo, makocha waliweza kuchangua wachezaji 16 ambao hana uhakika kuwa watawakilisha vyema Mkoa wa Lindi kwenye fainali za michuano hiyo ambazo zitafanyika Dar es Salaam kuanzia Septemba 6-11.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad