Mtaa Kwa Mtaa Blog

KANDANDA DAY 2016 KUCHANGISHA MADAWATI

TAMASHA la Kandanda maarufu kama ‘Kandanda Day’, linatarajia kufanyika Oktoba 15,  mwaka huu katika kiwanja cha Jakaya Kikwete Park (zamani Kidongo Chekundu).

Katika tamasha la mwaka huu,kauli mbiu itakuwa ni ‘Mpira na Dawati’ ikiwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kununua madawati yatakayogawiwa kwa shule mbalimbali nchini.

Mratibu wa tamasha hilo,Mohamed Mkangara,amesema kwamba mwaka huu wameamua kuja na kauli mbiu hiyo, ili kuunga mkono kampeni inayoendelea ya Serikali kuhusu madawati kwa shule za msingi na sekondari.
 “Umekuwa ni utaratibu wetu kila mwaka huu,kuja na kauli mbiu ambayo itahusisha soka na jambo ambalo moja kwa moja linaihusu jamii,kwahiyo, tumeona kwa kutumia soka,tunaweza kuisaidia jamii yetu kwa urahisi,”amesema  Mkangara

“Ndio maana kwa miaka yote tuliyofanya tamasha letu,kumekuwepo na ‘impact’ ya moja kwa moja kwa jamii inayotuzunguka,kwa hiyo ule utamaduni wetu tuliokuwa nao kwa miaka minne tunaendelea nao kwa mwaka huu kwa kukusanya fedha kwa ajili ya manunuzi ya madawati,ambapo tunatarajia kuchangisha fedha na kuuza jezi katika ‘dinner’ maalum ambayo tumeandaa kwa wadau mbalimbali.”
Mkangara,amesema kwamba madawati ambayo yatapatikana yatagawiwa kwa wawakilishi waliochaguliwa wa Kandanda kutoka mikoa mbalimbali nchini, ambao watahudhuria siku hiyo.

Tamasha la mwaka huu linatarajia kushirikisha timu mbalimbali alikwa,ukiacha timu wenyeji Time Dizo Moja na Timu Ismail.Pia,tamasha hilo linatarajiwa kupambwa na burudani mbalimbali na michezo ya kuvuta kamba kwa washiriki.
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget