HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, September 2, 2016

FIFA YAJA NA MFUMO MPYA WA GPX KURAHISISHA USAJILI

Na Zainab Nyamka

SHIRIKISHO  la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limezitaka klabu zote kujiunga na mfumo ujulikanao kama Global Players Exchange (GPX) ambao utarahisisha usajili wa mchezaji mmoja kwenda timu nyingine.

Mameneja wote wa usajili wa wachezaji kwa mfumo wa Mtandao (TMS-Transfer Matching System Managers) hawana budi kujiunga na mawasiliano mapya ili kupata taarifa mbalimbali za usajili na uhamisho wa wachezaji.

GPX ni kama mtandao wa kijamii unaoweza kulinganishwa na ‘WhatsApp’ unaofanya kuwa na mawasiliano ya karibu na FIFA imeagiza kuwa ni lazima mameneja wa TMS wa kila klabu na mashirikisho ya ya mpira wa miguu kujiunga na mtandao huo ambao si tu kwamba utafanya kazi katika nchi husika, bali pia unaunganisha ulimwengu wote.

Kwa mameneja wa usajili wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Ligi Daraja la Kwanza ya StarTimes (SFDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) watakaokuwa tayari basi hawana budi kuwasiliana na Meneja Usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kupata maelezo ya kina ya namna ya kujiunga na mtandao wa GPX.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad