HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 5, 2016

ASHANTI UNITED YAPIGWA TAFU NA BARAZA LA MADIWANI ILALA.

 Makamu Mwenyekiti wa Ashanti United United Almas Kasongo akizungumza na kueleza changamoto walizokuwa nazo katika kuendesha timu na kumshukuru Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko(kulia) kwa hatua nzuri waliyoifikia ya kuamua kuisaidia timu yao.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kayeko akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa timu ya Ashanti jijini Dar es Salaam.
  Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akizungumza wakati wa hafla iliyowakutanisha Baraza la Madiwani na Uongozi wa Ashanti United iliyofanyika mwishoni mwa wiki na kuisaidia timu hiyo kurejea ligi na itakuwa chini ya Manispaa ya Ilala                      
 Kulia ni Diwani wa kata ya Ilala, Saadi Khimji na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Ashanti United Almas Kasongo.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Ilala Charles Kuyeko ameitaka klabu ya Ashanti kuhakikisha wanarejea ligi kuu kwani kwa sasa wapo nao bega kwa bega.

Hatua hiyo imekuja baada ya Manispaa ya Wilaya ya Ilala kuona umuhimu wa kuwa na timu na sasa Ashanti itakuwa chini ya Manispaa na wataisimamia kwa hali na mali.

Akizungumza na Viongozi wa Ashanti pamoja na Baraza la Madiwani,  .Charles Kuyeko amesema Ashanti ni timu kubwa kwani ina muda mrefu sana na imeweza kuhimili kujiendesha kwa fedha chache za wanachama na zimekuwa hazitoshelezi kulingana na bajeti yao ya kila mwaka.

Kuyeko amesema kuwa kuna timu nyingi sana zinazosimamiwa na Manispaa na zimekuwa zikifa ya vizuri na zaidi ukiangalia kwa timu za Ilala zinazoshiriki  ligi daraja la Kwanza ukiacha Simba na Yanga zilizowafuata kuhitaji msaada wao zaidi ya Ashanti na baraza zima la madiwani wameahidi kushirikiana nao kwa hali na mali.

Kwa niaba ya uongozi wa Ashanti United, Makamu Mwenyekiti Almas Kasongo amesema kuwa wamepokea taarifa hiyo kwa bashasha kubwa sana hasa ukifikiria walikuwa na upungufu wa bajeti ya 2016/2017 ya takribani milioni 75, na zaidi ukiachilia hilo uwepo wa Baraza la Madiwani katika timu yao ya Ashanti utaleta hamasa kubwa sana kwa watu wengine kujitokeza kuja kuisaidia.

Ashanti United imeweza kuwakutanisha baraza la Madiwani wa Manispaa ya Ilala takribani 30 na wote wameonyesha nia ya kuiunga mkono timu hiyo na kwa kuanzia kwenye hafla hiyo, Mstahiki Meya alitangaza kuanza na Milioni tano lakini watakapokutana tena watasema ni kiasi gani watakitoa na watakapokuwa na shida wasisite kupiga hodi kwake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad