HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, October 2, 2015

VODACOM YAPATA TUZO YA KUWA MWAJIRI BORA NCHINI AFRIKA YA KUSINI

-Inaongoza katika sekta ya mawasiliano
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom imepata tuzo ya kuwa mwajiri bora katika sekta ya mawasiliano pia ipo miongoni mwa makampuni kumi bora yanayotoa ajira na kuwa na mazingira bora kwa wafanyakazi wake nchini Afrika ya Kusini kwa mwaka 2015.
Hafla ya kutangaza makampuni yanayoongoza kwa ajira nchini Afrika ya Kusini ilifanyika jana katika eneo la Gallagher Estate mjini Jahannesburg ambapo Vodacom ilitangazwa kuwa miongoni mwa makampuni 10 bora yanayoongoza katika ajira na kwa kufuata taratibu na kanuni za raslimali watu na ilitangazwa kuwa kampuni inayoongoza kwa kufuata misingi bora ya ajira katika sekta ya mawasiliano.
Tuzo ya waajiri bora ni mpango ambao uandaliwa kila mwaka na makampuni yanayoongoza kwa kufuata sheria na misingi bora ya ajira na raslimali watu hutangazwa na kupewa tuzo.
Akiongea baada ya kupata tuzo hiyo Afisa Mtendaji Mkuu wa raslimali watu wa Vodacom Matimba Mbungela alisema:”Tumewekeza kwa kisi kikubwa katika uendeshaji wa shughuli za raslimali watu katika kampuni yetu kuanzia teknolojia na kuweka mifumo bora inayokubalika kimataifa  ambayo inatoa mwanya kwa wafanyakazi wetu kufanya kazi katika mazingira mazuri na kampuni kuendesha shughuli zake kwa ufanisi mkubwa”.
Mbungela alisema kuwa tuzo hii  inatoa taswira halisi ya kampuni yetu kwa kuwa kuwa mwajiri bora kunaendana sambamba na kutoa huduma bora kwa wateja.
Tuzo hii imetolewa kwa Vodacom baada ya kubainika kuwa inafuata  na kutekeleza kanuni na taratibu za raslimali watu zinazokubalika kimataifa na imekuwa mstari wa mbele kuajiri wafanyakazi wazuri na kuendeleza vipaji vyao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad