TAREHE 26-9-2015 jana jumamosi kulifanyika mechi ya ligi
kuu ya vodacom Tanzania bara baina y a klabu yetu ya Simba na timu ya
Yanga.
Kwenye mchezo huo timu yetu imepoteza mchezo huo kwa kufungwa goli mbili kwa bila.
Tumeanza kuandika hvyo hapo juu kwa maksudi kuonyesha sisi
Simba tumeyakubali matokeo hayo ya dakika tisini za mchezo na tutumie
nafasi hii kiungwana kabisa kuwapongeza watani wetu wa jadi kwa ushindi
huo walioupata.
Pili tumshukuru mungu kwa kutuwezesha kumaliza mchezo huo salama na
hapa mungu ashukuriwe sana pamoja na wapenzi wetu pia.sababu washabiki
wetu wameonyesha utulivu wa kiunamichezo kwa kutokufanya fujo yoyote
licha ya mwamuzi wa mchezo huo Israel Nkongo kuharibu mchezo kwa
makusudi.
Nkongo kwa dhamira ya kusudi jana aliamua kuwatoa wachezaji
wetu mchezoni kwa kuanza kugawa kadi kwa wachezaji wetu pasi na sababu
na kwa rafu zilezile kuacha wachezaji wa Yanga kucheza bila kuwaonya.
Kilichoshangaza washabiki wote waliokuwa uwanjani na walioangalia kwenye
televisheni ni kumuacha mchezaji wa Yanga Donald Ngoma kuendelea na
mchezo ilhali alimpiga kichwa cha maksudi mchezaji wetu Hassan kessi!!
Mbali ya vitendo hvyo wachezaji wetu wametulalamikia kutukanwa na mwamuzi wa mchezo huo Nkongo.
Tunaamini Tff watachunguza malalamiko yetu na kuchukua hatua stahiki kwa
mwamuzi huyo ambaye kila mtu aliyeuona mchezo huo anakiri kuwa
alishindwa kuumudu.
Mwisho na kwa umuhimu wa kipekee klabu ya Simba inaendelea
kuwashkuru washabiki kwa utulivu wao licha ya vitendo vya mwamuzi huyo
ambavyo vingeweza kabisa kuharibu amani iliyokuwepo uwanjani jana.
Tunawaomba waendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki ambacho uongozi
wenu umewaandikia TFF na bodi ya ligi ambazo tunaamini zitatenda haki..
Reclaming our glrory
Simba nguvu moja
Imetolewa na Haji S.Manara
Mkuu wa habari wa Simba
Simba sports club
27-9-2015
Nb.mchezo dhidi ya yanga ushapita na sasa tunajipanga kwa game ijayo.
Tunawaomba wapenzi wetu mjitokeze kwa wingi kwenye mechi yetu dhidi ya Stand united jtano ijayo ya tarehe 30-9-2015

No comments:
Post a Comment