93.7 EFM yajinyakulia ushindi baada ya kuwafunga kibaha veterans mabao mawili kwa moja, katika mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Tamco kibaha, Mechi hiyo ni baadhi ya mechi zinazoendelea baina ya EFM na timu mbalimbali za wasikilizaji wake, Kupitia kampeni ya Muziki mnene bar kwa bar .
Burudani haikuishia hapo, baada ya mechi hiyo shangwe ziliendelea ndani ya kibaha kontena. Ilikuwa ni bandika bandua ya ngoma kali kutoka kwa Rdj’s wa 93.7 EFM na shamra shamra kutoka kwa timu nzima ya EFM na wakazi wa kibaha.



No comments:
Post a Comment